Breaking News

Your Ad Spot

May 20, 2015

MBUNGE WA JIMBO LA TEMEKE ABBAS MTEMVU AFANYA ZIARA YA UKAGUZI WA MAENEO YALIYOHARIBIWA NA MVUA.BAADHI YA MAENEO HAYO NI SOKO LA TAZARA NA DEVIS CONER

  Diwani wa Soko la Tazara Vetenary Zahoro Maganga akitoa maelezo kwa Mbunge wa Jimbo la Temeke Abbas Mtemvu alipotembelea maeneo yaliyoharibiwa  na mvua akiongozana na  viongozi wa Wakala wa Serikali wa Barabara (Tanroads) jinsi maji yanavyotakiwa kufata mfereji huo ambao haupitishi maji kupeleka katika mfereji huo  (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)

 Mbunge wa Jimbo la Temeke Abbas Mtemvu (kulia) akizungumza na viongozi wa Wakala wa Serikali wa Barabara (Tanroads)  katika ziara ya kutembelea maeneo yaliyo haribiwa na mvua zilizokuwa zikiendelea kunyesha Jijini Dar es Salaam (kushoto) ni Meneja wa Tanroads Mkoa wa Dar es Salaam, Mhandisi Julius Ndyamukama.
 Mhandisi Mradi Tanroads Mkoa wa Dar es Salaam Ngusa Julius (wa pili kulia)  akimwelekeza jambo Mbunge wa Jimbo la Temeke Abbas Mtemvu (aliye vaa kofia) wakati wa ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali ya jimbo lake yaliyo haribiwa na mvua na kusaidia kutowa Mashine ya kuondoa  maji hayo yaweze kuondolewa (kushoto) ni Katibu wa Kamati ya maafa na miundombinu ya Soko la Vetenary Manispaa ya Temeke  Morocco Milanzi na kulia ni Naibu Meya Manispa  Temeke Juma Mkenga
Katibu wa Kamati ya maafa na miundombinu ya Soko la Vetenary Manispaa ya Temeke  Morocco Milanzi (wapili kulia) akizungumza na viongozi wa Wakala wa Serikali wa Barabara (Tanroads) wakiongozwa na Mbunge wa Jimbo la Temeke Abbas Mtemvu (wa pili kushoto), wakati wa  ziara ya kutembelea maeneo yaliyo haribiwa na mvua zilizokuwa zikiendelea kunyesha Jijini Dar es Salaam na mbunge huyo kusaidia mashine ya kuyaondosha maji hayo
 Baadhi ya maeneo waliyo kumbwa na maji katika  Soko la Vetenary Manispaa ya Temeke
Meneja wa Tanroads Mkoa wa Dar es Salaam, Mhandisi Julius Ndyamukama akiwa na (wa tatu)kulia akizungumza jambo wakati wa ziara na Mbunge Abbas Mtemvu wakati wa ziara hiyo
Mwenyekiti wa Serikali ya Mta wa Kilimahewa Tandika Devis Coner  Mfaume Mbonde (kulia)  akielekeza jambo wakati wa  ziara ya Mbunge na viongozi wa Tanroads wakiangalia maeneo yaliyoharibiwa na mvua nakuahidi kufanyia marekebisho maeneo hayo

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages