Michuano ya kumi na tano ya Baraza
la Vyama vya Mpira wa Miguu kusini mwa Afrika,COSAFA imezikutanisha timu
za ukanda huo nchini Afrika Kusini. Michuano hiyo ilianza kutimua vumbi
Jumapili mei 17 na itakamilika mei 30
Timu 12 kati ya 14 kutoka
nchi wanachama wa COSAFA tayari zipo nchini Afrika Kusini kuchuana
katika mashindano hayo. Angola na Comoro ambazo ni wanachama wa COSAFA
hazikuweza kushiriki mwaka huu.
Nafasi zao zimechukuliwa na Ghana
iliyofikia fainali za michuano ya Caf ya mwaka huu na Tanzania kutoka
ukanda wa Afrika mashariki na kati ikiwa mwanachama wa CECAFA.
Timu
nane zenye viwango vya chini kwa ubora kwa mujibu wa takwimu za FIFA
kwa mwezi Februari, zimepangwa katika makundi mawili yenye timu nne kila
moja, Tanzania ikiwemo katika michuano hiyo.
Kundi A lina timu za
Zimbabwe, Namibia, Seychelles na Mauritius. Ambapo kundi B lina timu za
Madagascar, Lesotho, Swaziland na Tanzania.
Katika kundi A
Zimbabwe inaoongoza kundi hilo kwa kujikusanyia pointi sita baada ya
michezo miwili ikifuatiwa na Namibia yenye pointi nne. Seychelles ni ya
tatu na pointi moja. Mkiani ni Mauritius ambayo haina pointi.
Na katika kundi B, Madagascar na Swaziland zote zina pointi tatu, huku Lesotho na Tanzania zikiwa mikono mitupu.
Tanzania
leo,Jumatano inarusha karata yake ya pili kwa kupambana na Madagascar
baada ya kucharazwa bao 1-0 na Swaziland katika mchezo wake wa kwanza.
Timu
za juu katika kila kundi zitasonga mbele hatua ya mtoano, ambapo timu
sita za viwango vya juu zitaingia katika mashindano hayo yakiwa katika
hatua ya robo fainali na kuendelea. Afrika Kusini kutokana na ubora wake
itapambana na Botswana hatua ya robo fainali.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269