Shirikisho la soka barani Ulaya linajiandaa kuondoa sheria ya mwaka 2011 itakayozuia vilabu kufanya matumizi ya ziada.
Katika
mahojiano na redio ya Ufaransa RTL,rais wa UEFA Michel Platini amesema
kuwa sheria hiyo ilikuwa ikifanya kazi vizuri lakini itapigwa msasa
mishoni mwa msimu huu. Hatua hiyo inafuatia ripoti katika gazeti
la Le Parisien siku ya jumapili iliosema kuwa kuna mabadiliko muhimu
yatakayofanyiwa sheria hiyo. Manchester City pamoja na kilabu ya PSG zilipigwa faini mwaka uliopita kwa kukiuka sheria hiyo. Baadaye
mwandani wa rais wa vilabu vya Ulaya ambaye pia ni katibu mpanga ratiba
Gianni Infantino aliithibitishia BBC kwamba mazungumzo kuhusu FFP na
vilabu vikuu vya Ulaya yanaendelea huku marekebisho hayo yakijadiliwa
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269