Na Miza Othman- Maelezo Zanzibar
Serikali ya awamu ya saba imechukuwa hatuwa mbambali za kuimarisha huduma za Elimu, Afya,Majisafi na salama pamoja na Makaazi ili kuleta ustawi mzuri kwa jamii.
Hayo yameeelezwza leo na Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi (pichani), wakati akiwasilisha hutuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Makamu wapili wa Rais kwa Mwaka wa Fedha 2015/2016 huko Chukwani katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Amesema Serikali imeendelea kuchukuwa hatuwa madhubuti ya kuimarisha na kuendeleza elimu ikiwemo ujenzi wa Skuli na Madarasa mapya kwa Skuli za Maandalizi Msingi na Sekondari, pamoja na Ununuzi wa Vitabu vya ziada katika Skuli mbali mbali za Unguja na Pemba.
Balozi Seif amesema Serikali itaendelea kuwajengea uwezo Walimu kwa kuwapatia mafunzo ya muda mrefu na mfupi kwa lengo la kuimarisha ubora wa Elimu inayotolewa Maskulini humo.
Aidha amesema pia Serikali itaendelea kuimarisha huduma za kinga na Tiba katika Hospitali na Vituo vya Afya sambamab na kutowa Elimu ya Afya kwa Wananchi kwa lengo la kujikinga na maradhi ya kuambukiza na yasioambukiza.
Hata hivyo amesema Serikali imezifanyia matengenezo makubwa Hospitali na Vituo vya Afya na kujenga Majengo mengine mapya Unguja na Pemba ikiwemo Wodi ya wagonjwa mahatuti (ICU) na kitengo cha huduma za upasuwaji Vichwa na Uti waMgongo (Neuro Surgical Unit) katika Hospitali ya Mnazi Mmoja.
Vile vile Serikali imechukuwa Madaktari na Wahudumu wengine wa Afya kwa kuwasomesha na kuwapatia uzowefu kutokana na Nchi kwani hivi sasa inamadaktari wazalendo.
“Hivi sasa Nchi yetu inamadakatari wazalendo wapatao 44 na Madaktari Bingwa wazalendo 13”, amesema Balozi Seif .
Kutokana na hali hiyo Serikali imesema kwamba imeshawapatia Madaktari wa Maradhi mbali mbali kwa lengo la kuwahudumia Wananchi kwa kushirikiana na Nchi marafiki.

No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269