Timu ya
Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imewasii salama leo alfajiri ikitokea
nchini Afrika Kusini ilipokua ikishiriki michuano ya Kombe la Cosafa,
baada ya kutolewa katika hatu ya awali ya makundi.
Stars
ambayo jana jioni ilipoteza mchezo wake wa mwisho dhidi ya Lesotho baada
ya kufungwa bao 1 - 0, imerejea baadaa ya kupoteza michezo yote mitatu
ya kundi B, baada ya kufungwa na Swaziland, Madagascar na Lesotho.
Mara
baada ya mchezo wa jana dhidi ya Lesotho, kocha mkuu wa Taifa Stars Mart
Nooij alisema amesikitishwa na matokeo ya timu yake katika hatua hiyo
ya awali baada ya kupoteza michezo yote mitatu.
Nooij
alisema, mpira wa miguu umebadilika kwani matarajio yake yamekua
tofauti, kwani kiwango walivyoonyesha wapinzani wake katika kundi B
vimemstajaabisha.
“Mpira wa
sasa hautazami nani yupo juu katika renki za FIFA, tulikua na matarajio
ya kufanya vizuri katika michuano hii lakini baada ya dakika ya 90 za
kila mchezo matokeo hayakua mazuri kwetu” alisema Nooij”
Kuhusu
kufuzu kwa AFCON 2017, Nooij amesema katika kikosi chake alichokwenda
nacho Cosafa alikua na wachezaji saba aliowapandisha, anaamini wamepata
uzoefu, na sasa atawajumuisha na wachezaji ambao hawakuweza kushiriki
michuano hiyo kujiandaa na mchezo dhidi ya Misri.
Taifa
Stars inatarajia kucheza kucheza mchezo wake wa kwanza wa kuwania kufuzu
kwa AFCON 2017 dhidi ya Misri, tarehe 14 Juni 2015 katika uwanja wa
Borg el Arab jijini Alexandria.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269