Saudia
Takriban
watu kumi wamekufa katika shambulizi la mlipuaji wa kujitolea muhanga
katika msikiti mmoja wa Shia mkoa wa mashariki wa taifa la Saudi Arabia
,kulingana na daktari mmoja.
Daktari
wa kukabiliana na dharura katika hospitali ya Qatif amesema kuwa
takriban watu sabini wamejeruhiwa huku wengine wakijeruhiwa vibaya.
Walioshuhudia wameripoti mlipuko mkubwa katika msikiti wa Imam Ali uliopo katika kijiji cha al-Qadeeh,katika jimbo la Qatif.BBC
Saudia
Ni kisa
cha kwanza cha aina hiyo kutokea Saudi Arabia huku kukiwa na mvutano
katika eneo hilo kati ya waislamu wa madhehebu ya Sunni na Shia.
Kundi la
Islamic State limedaiwa kutekeleza shambulizi kama hilo katika taifa
jirani la Yemen siku ya ijumaa ambalo liliwajeruhiwa watu kadhaa.
Hatahivyo
halijatoa tamko lolote kuhusu shambulizi la bomu mashariki mwa Saudia
na hakuna kundi jingine lolote lililojihusisha na shambulizi hilo.
Saudia msikiti
Picha za runinga ya kundi la Hezbolla al-Manar zilionyesha vioo vilivyovunjika pamoja na vifusi ndani ya msikiti.
Miili iliozibwa na nguo ilionekana imetapakaa katika sakafu ya msikiti huo.
Watu wa
dhehebu la Shia walio wachache wanaishi mkoa wa mashariki na kumekuwa na
malalamishi ya washia wanaotaka kupewa haki zaidi.
Saudia msikiti
Hili ni shambulizi la kwanza lililotekelezwa katika msikiti wa Shia.
Tukio
hilo linajiri huku muungano wa majeshi unaoongozwa na Saudi Arabia
ukiendeleza kampeni yake dhidi ya waasi wa kishia katika taifa jirani la
Yemen.
Msikiti saudia
Taifa la Saudi Arabia pia limetishwa na Islamic state ambalo linalengwa na muungano wa kimataifa iwemo ufalme huo wa kisunni.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269