Waandamanaji
katika mji wa Bujumbura.
Watu watatu wameuawa katika milipuko ya guruneti jijini kati Bujumbura, Mei 22 mwaka 2015. mouvement en aidant donnant de l'eau aux manifestants.
Watu watatu wameuawa katika milipuko ya guruneti jijini kati Bujumbura, Mei 22 mwaka 2015. mouvement en aidant donnant de l'eau aux manifestants.
Na RFI
Watu
watatu wameuawa na wengine zaidi ya ishirini wamejeruhiwa katika
milipuko mitatu ya guruneti ziliyorushwa kwenye kituo cha mabasi jijini
kati Bujumbura leo Ijumaa jioni. Waliondesha mashambulizi hayo
hawajulikani.
Idadi hiyo ya watu waatu waliopoteza maisha huenda ikaongezeka.
Idadi hiyo ya watu waatu waliopoteza maisha huenda ikaongezeka.
Wakati
huo huo maandamano yameendelea leo Ijumaa katika wilaya mbalimbali za
jiji la Bujumbura. Maandamano hayo yameendelea wakati ambapo mkurugenzi
na mmiliki wa kituo cha redio na telivisheni Rennaissance Fm, Innocent
Mohozi amesikilizwa kwenye Ofisi ya mashataka.
Rennaissance
Fm ni moja ya vyombo vya habari binafsi vilivyoshambuliwa na kuchomwa
moto wakati wa jaribio la mapinduzi, juma moja lililopita.
Innocent
Muhozi amesikilizwa kwa muda wa masaa 4, lakini aliruhusiwa kurejea
nyumbani kwake. Afisaa wa mashtaka amemsikiliza mkurugenzi huyo katika
lengo la kuendesha uchunguzi kuhusu jaribio la mapinduzi.
Ofisi ya
mashtaka imemuhoji mkurugenzi wa kituo cha redio na televisheni
Rennaissance Fm kuhusu kurushwa hewani kwa tangazo la jenerali Godefroid
Niyombare la mapinduzi ya serikali, Jumatano wiki iliyopita.
Mpaka
hatua hii Innocent Muhozi ana imani kuwa hatorudi kufuatiliwa na vyombo
vya sheria, lakini ana hofu kuwa huenda vyombo vya sheria vikashinikizwa
kutumia mbinu nyingine.
"
Uchunguzi umeanzishwa, nina imani kuwa sintorudi kufuatiliwa, kwani
tulitekeleza kazi yetu ya uandishi wa habari ", amesema Innocent Muhozi.
Mpaka sasa Innocent Muhozi hajaikimbia nchi yake wala kuingia mafichoni kama wakurugenzi wa vituo vya redio binafsi vingine.
Mkurugenzi
huyo wa kituo cha redio na runinga binafsi Rennaissance Fm ameeleza
kuwa polisi ndio iliyovamia na kuchoma moto majengo ya kituo chake cha
redio na runinga Rennaissance Fm.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269