Rais Omar al Bashir wa Sudan amewasili mjini Khartoum Sudan kutoka nchini Afrika Kusini. Rais Bashir amekariri kuwa hana hatia yeyote wala hajui kwanini mahakama ya kimatiafa ya ICC inasisitiza kumchafulia jina.
Shirika la habari ya AFP limemnukuu rais Bashir akifoka ''Allah Akbar'' aliposhuka kutoka kwa ndege iliyombeba. Aidha aliinua mkongojo wake juu na kushabikiwa na wafuasi wake.
Waziri
wa maswala ya kigeni wa Sudan Ibrahim Ghandour aliwaambia waandishi wa
habari kuwa serikali ya Afrika Kusini ilikuwa imemkariria rais Bashir
kuwa kuwepo kwake mjini johannesburg ilikuwa ni tukio la kushabikiwa na
lenye heshima kubwa kwa hivyo hakukuwa na uwezekano wowowte wake
kukamatwa.
Rais Huyo alikuwa ameratibiwa kuhutubia umma lakini kinasa sauti
kikaharibika na akaondoka. Rais bashir aliingia katika gari lake lililowazi na akaondoka
uwanjani huku akishabikiwa na wafuasi wake.
Awali kuondoka kwake nchini Afrika Kusini kulikumbwa na atiati,
baada ya mahakama moja kuamuru rais huyo asiondoke nchini humo hadi mahakama
hiyo itakaposikiza kesi na kuamua iwapo atakamatwa na apelekwe mjini the Hague
Uholanzi au la.
Awali Mwandishi wa BBC aliyeko Afrika Kusini Nomsa Maseko,
alisema kuwa ndege ya rais al Bashir ilijazwa mafuta jana usiku na kuwekwa
mstari wa mbele tayari kabisa kuondoka katika uwanja wa ndege wa kijeshi.
Rais Bashir aliondoka licha ya kuwepo amri ya mahakama ya
kumzuia kuondoka nchini humo hadi kesi dhidi yake itakaposikizwa na kuamuliwa.
Mahakama hiyo ilikuwa inapaswa kuamua ikiwa Bwana al-Bashir
atakabidhiwa mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai ICC yenye makao yake
mjini Hague Uholanzi ilikukabiliana na mashtaka ya uhalifu wa kivita na mauaji
yahalaiki yanayomkabili .
Majaji watatu waliokuwa wanasikiza kesi hiyo dhidi yake
wamemtaka waziri wa usalama wa ndani nchini humo kueleza ni vipi rais Bashir
aliruhusiwa kukaidi amri ya mahakama
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269