Mkurugenzi
Mtendaji wa Makampuni ya Dangote, Alhaji Aliko Dangote, akizungumza na
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Hawa Ghasia alipowasili
kwenye uwanja wa Ndege mjini Mtwara jana kwa ajili ya kutembelea kiwanda
chake cha Cementi kilichoko Msijute, mkoani Mtwara.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, Hawa Ghasia akiteta jambo na
Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Dangote, Alhaji Aliko Dangote,
alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Mtwara leo kwa ajili ya kuangalia
maendeleo ya ujenzi wa kiwanda cha Cementi cha Dangote. Katikati ni
Balozi wa Nigeria Nchini Tanzania, Ishaya Manjanbu.
Mkurugenzi
wa Makampuni ya Dangote, Alhaj Aliko Dangote (kulia), akijadiliana
jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka,
walipokutana mjini Mtwara jana kuangalia uwezekano wa kujenga kituo cha
kusafirisha saruji katika eneo la Bandari ya Mtwara.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Makampuni ya Dangote, Alhaji Aliko Dangote, akizungumza na
waandishi wa habari baada kuwasili mjini Mtwara jana na kutembelea
kiwanda chake cha Cementi, kilichoko Msijute, mkoani Mtwara.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Makampuni ya Dangote, Alhaj Aliko Dangote akisaini kitabu
cha wageni, baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege mjini Mtwara jana,
kwa ajili ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kiwanda chake cha saruji.
Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka.
Mkurugenzi
wa Makampuni ya Dangote, Alhaj Aliko Dangote akiwafuatana na wenyeji
wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Hawa Ghasia (wa pili kushoto),
Balozi wa Nigeria, Ishaya Manjanbu (wa pili kulia) na Mkuu wa Wilaya ya
Mtwara, Bi. Fatma Salum Ali (kushoto), alipowasili kwenye uwanja wa
ndege, mjini Mtwara jana.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Makampuni ya Dangote, Alhaj Aliko Dangote, akiteta jambo na
Mwakilishi mkazi wa Dangote nchini Tanzania, Bi. Esther, mjini Mtwara ,
baada ya Mkurugenzi huyo kutembelea kiwanda chake cha saruji
kinachojengwa mkoni Mtwara.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269