Breaking News

Your Ad Spot

Jun 18, 2015

CRDB TAWI LA MERU WATEMBELEA KITUO CHA YATIMA ST JOSEPH CHA MOSHONO ASRUSHA



 Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Meru jijini Arusha  Leonce Matley akikabidhi  misaada kwa Mkurugenzi wa kituo cha watoto yatima cha St.Joseph Christina Mnate juzi walipotembelea kituo hicho na kutoa misaada ya chakula na vifaa vya shule katika kituo hicho kilichopo kata ya Moshono jijini Arusha ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya Mtoto Afrika .
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Meru jijini Arusha  Leonce Matley akikabidhi  misaada kwa Mkurugenzi wa kituo cha watoto yatima cha St.Joseph Christina Mnate juzi walipotembelea kituo hicho na kutoa misaada ya chakula na vifaa vya shule katika kituo hicho kilichopo kata ya Moshono jijini Arusha ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya Mtoto Afrika 
******************
JUKUMU la malezi ya watoto yatima na waishio katika mazingira magumu nchini linapaswa kutekelezwa na kila mtanzania pamoja na tasisi mbalimbali nchini ili kupunguza wimbi la wananchi tegemezi.

Hayo yalisema na Meneja wa Benki ya CRDb tawi la Meru, Leonce Matley, wakati wa kukabidhi msaada wa vitu mbalimbali katika kituo cha watoto yatima na waishio katika mazingira magumu cha St.Joseph kilichopo Kata ya Moshono jijini Arusha. 

“Malezi ya watoto hawa yatima ni jukumu letu sote kama  watanzania  kuhakikisha kuwa tunawasaidia watoto yatima na wanaoishi mazingira magumu ili waweze kupata elimu bora itakayowakomboa kimaisha,” alisema Matley.

CRDB ilitembelea kituo hicho ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika iliyoadhimishwa dunai kote hivi karibuni ambapo wafanyakazi wa benki walipata wasaa wa kufurahi na watoto hao pamoja na kutoa misaada ya vyakula na vifaa vya shule katika kituo hicho ikiwa ni njia mojawapo kuwezesha upatikanaji wa mahitaji ya watoto yatima.

Aidha Matley amezitaka taasisi mbalimbali zilizopo nchini na asasi za kiraia kujaribu kujitoa kwa moyo kusaidia kundi hili la jamii ambalo likipata makuzi mazuri na salama litaweza kujiongoza lenyewe hapo baadae pasipo misaada zaidi hasa wakipatiwa mazingira mazuri ya kupata elimu.

Nae Mkurugenzi wa Kituo cha watoto yatima cha St.Joseph, Sister Mary Mushi  ametoa shukrani kwa uongozi wa benki hiyo kwa msaada walioupata na kutaka kuendelea kufanya hivyo kila wapatapo nafsi kwani huwapa faraja watoto hao.

“Nijambo la kumshukuru Mungu kwa moyo aliowapa wa kijitolea na kutukumbuka, na hili jamii isiyaachie tu makampuni kama CRDB bali hata mtu mmoja mmoja anaweza kuwasaidia yatima hawana kuwapa malezi bora badala ya kuwaachia wageni kutoka nchi za nje  ili kujenga taifa imara,”alisema Sister Mushi.

Siku ya Mtoto Afrika huadhimishwa kila mwaka June 16 katika nchi za Afrika huku Changamoto kubwa ya ongezeko la watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu ikiongezeka kutokana na mimba za utotoni.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages