Pichani
ni Mhudumu wa Mapango ya Chinhoyi Cephas Sithole akitoa maelezo kwa
timu ya waandishi wa habari waliombatana na wadau wa utalii kutoka
nchini Afrika Kusini kwenye ziara hiyo ya kutembelea vivutio vya utalii
nchini Zimbabwe katika mapango Chinhoyi.(Picha zote na Zainul Mzige).
Na Modewjiblog team, Harare
Waandishi
wa habari kutoka vyombo 5 vya habari vya magazeti ya Tanzania ikiwemo
mtandao wa habari wa modewjiblog ambao ni Justin Damiana (The African),
Frank Aman (The Guardian), Zainul Mzige (modewjiblog),
Mariam Said (Daily News) pamoja na Timothy Kitundu (East Africa
Business Week) walipata mwaliko kutoka Mamlaka ya Utalii ya Zimbabwe
(ZTA) kufanya utalii katika mapango ya Chinhoyi, Ziwa Kariba, Shamba la
ufagaji wa Mamba, Hifadhi ya Taifa ya Kariba, Bandari ya Zambezi pamoja
na ukuta wa bwawa la Kariba unaotengenisha nchi ya Zambia na Zimbabwe.
Safari
ya kuelekea nchini Zimbabwe ilidhaminiwa na Shirika la usafiri wa Anga
wenye gharama nafuu Fastjet Tanzania ikiwa ni moja ya mipango yao ya
kuimarisha safari zake za kutoka Dar es Salaam-Lusaka na Harare.
Safari
hiyo ilikuwa maalum kwa ajili kuhudhuria maonyesho ya naneya Kimataifa
ya Utalii Sanganai/Hlanganani–(World Tourism Expo) ambayo yameanza
kurindima jijini Harare katika ukumbi wa Harare International Conference
Centre (HICC).
Mungoza
watalii katika mapango ya Chinhoyi katika mkoa wa Chinhoyi nchini
Zimbabwe, Aleck Makumire akitoa maelezo wa timu ya waandishi wa habari
kabla ya kushuka kwenye mapango hayo wakati wa ziara maalum ya
kutembelea vivutio vya Utalii nchini humo.
Mungoza
watalii katika mapango ya Chinhoyi katika mkoa wa Chinhoyi nchini
Zimbabwe, Aleck Makumire akiwa ndani ya mapango ya Chinhoyi akitoa
maelezo kwa waandishi wa habari wa Tanzania katika ziara yao ya
kutembelea vivutio vya utalii nchini humo.
Waandishi
wa habari kutoka Tanzania waliosafirishwa na Shirika la ndege lenye
gharama nafuu nchini Fastjet kuhudhuria maonyesho ya Kimataifa ya Utalii
ya Shanganai yanayoendelea nchini Zimbabwe. Kutoka kushoto ni Timothy
Kitundu (East Africa Business Week), Mariam Said (Daily News) pamoja na
Justin Damiana (The African) wakiwa wameketi kwenye mapango ya Chinhoyi
huku wakibadilishana mawazo na wadau wa utalii kutoka Afrika Kusini.
Wakirejea
kutoka kwenye mapango hayo ambayo chini yana maji ambayo hayatembei
wala kukauka. (pichani kwa chini yakionekana kuwa na rangi ya bluu
lakini ukichota ni meupe).
Mwandishi
wa habari Timothy Kitundu (East Africa Business Week) akitoka kudhuru
mapango hayo wakati wa ziara ya kutembelea vivutio vya utalii.
Rumbidzai
Mudzengerere wa Mamlaka ya Utalii ya Zimbabwe (ZTA) akifurahia ukodak
wa kamre ya modewjiblog akitokea ndani ya mapango ya Chinhoyi. Kulia ni
Mwambata wa Waziri wa Utalii anayehusika na masuala ya uhamiaji kwa
Afrika nchini Zimbabwe, Sherry Sibanda.
Picha ya pamoja na wenyeji wetu.
Ziara ya waandishi kutembelea kanisa la Mtakatifu Barbara.
This
delightful little round church situated above Kariba town on the hill
known as Kariba Heights, was built by workers and engineers employed by
Impresit, the Italian company contracted to build the Kariba dam wall.
The church is dedicated to St Barbara, who is the patron saint of
engineers/construction workers.
On
the outside walls of the church is a dedication in Latin to the memory
of the construction workers killed during the building of Kariba Dam and
a plaque with the names of those who lost their lives is found inside.
The church has beautiful stained glass windows and an open-air design
which is perfectly suited to the hot climate of Kariba. A bell tower at
the back of the church still contains the original bell constructed by
hand by Italian workers at the time and hoisted into place with a crane.
Read the detailed story about the church bell of Santa Barbara at this link: The Bell of Santa Barbara Church: A Modern Legend in the Making
Picha ya kumbukumbu nje ya kanisa hilo.
Kulia ni Meneja mwendeshaji wa mtandao wa habari wa modewjiblog, Zainul Mzige akiwa ameambatana na waandishi wenzake kwenye ziara hiyo.
Sehemu ya muonekano wa Ziwa Kariba kwa juu zinapopaki boti za utalii za watu binafsi na makampuni.
Kutoka kushoto ni Timothy Kitundu, Mariam Said na Justin Damian wakipata ukodak wakati wa ziara hiyo ya Kariba.
Muonekano wa Ziwa Kariba.
Muonekano wa ukuta wa bwawa la Kariba unaotengenisha nchi ya Zambia na Zimbabwe.
Meneja mwendeshaji wa mtandao wa habari wa modewjiblog, Zainul Mzige akitazama ukingo wa ukuta huo wakati wa ziara ya Kariba nchini Zimbabwe.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Going Places Tours & Travel ya Zambia, Rachel Ward
akipozi na Mwambata wa Waziri wa Utalii anayehusika na masuala ya
uhamiaji kwa Afrika nchini Zimbabwe, Sherry Sibanda kwenye meli kubwa ya
kitalii inayotumika kutembeza watalii ambayo inalaza zaidi ya watu 50
huku ikiwa na sehemu ya ukumbi wa burudani na wakati mwingine hukodiwa
kama ukumbi wa harusi ndani ya maji pamoja na baadhi ya vyumba maalum
kwa wanandoa wanaoenda mapumzikoni (Honey moon).
Sherry Sibanda na Captain wa muda Zainul Mzige wakipata ukodak ndani ya meli hiyo.
Captain wa muda Frank Aman akipozi kwa ukodak.
Captain wa muda Timothy Kitundu ndani ya meli.
Muonekano wa Meli hiyo.
Usalama
Kwanza: Mariam Said (Daily News) akivaa boya kabla ya kuanza safari ya
kuzunguka ziwa Kariba na kulia ni Victoria Siphiwe Mamvura Gava
akisaidiwa kuvaa boya na Nahodha ya boti hiyo.
Kutoka
kushoto ni Victoria Siphiwe Mamvura Gava, Cherry Sibanda na Mariam Said
wakiwa wamepumzika huku wakipitia baadhi ya vipeperusha vya boti za
kitalii zinazokodishwa kwa ajili ya kupumzika katika ziwa la Kariba.
Kundi jingine likiwa kwenye ziara ya ziwa Kariba likiongozwa na Rumbidzai Mudzengerere wa Mamlaka ya Utalii ya Zimbabwe (ZTA).
Kituo cha mafuta katika Bandari ya Marine Land kikiwa ndani ya Ziwa Kariba.
Boti
ya Matusadona inayokodishwa kwa watalii ambapo kila kichwa ni $5000 kwa
usiku mmoja ambayo ina uwezo wa kubeba watu saba pamoja na mpishi
maalumu kwa ajili ya kuwapikia chakula.
Viboko ndani ya Ziwa Kariba.
Wanahabri wakirejea baada ya ziara ya kuzunguka Ziwa Kariba.
Timu
ya waandishi wa habari kutoka Tanzania wakipiga picha katika shamba la
Mamba la Padenga ambalo ni shamba kubwa la ufugaji wa Mamba kuliko yote
kusini mwa Afrika.
Baadhi ya Mamba wakiwa mapumziko ndani ya shamba hilo.
Mmoja wa Mamba akiwa ametega Nzi wajae ndani ya mdomo wake.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269