Mkurugenzi Mtendaji wa Lotus Clinic, Dialla Kassam (katikati), akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, wakati wa uzinduzi wa kampeni maalum ya kueneza uelewa kuhusu tatizo la usonji ‘Autism’ nchini Tanzania iliyondaliwa na Lotus Medical Clinic kwa
kushirikiana na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na taasisi ya Autism Education Trust ya Uingereza. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Kuhudumia watu wenye Usonji Tanzania, Dk. Stella Rwezaula na Daktari wa kufundisha kuongea, Nazreem Sumar.
Mkurugenzi Mtendaji wa Lotus Clinic, Dialla Kassam (katikati), akitoa utambulisho kwa meza kuu mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana katika uzinduzi huo. Kushoto ni Mtaalam wa Afya kutoka taasisi ya Autism Education Trust ya Uingereza, Kevin Baskerville, Mwenyekiti wa Chama cha Kuhudumia watu wenye Usonji Tanzania, Dk. Stella Rwezaula (wa pili kushoto), Daktari wa kufundisha kuongea wa Lotus, Nazreem Sumar (wa pili kulia) na Daktari Fathema Hasham.
Mkurugenzi Mtendaji wa Lotus Clinic, Dialla Kassam.
Mtaalam
wa Afya kutoka taasisi ya Autism Education Trust ya Uingereza, Kevin
Baskerville (kushoto) akipongezana na Mwenyekiti wa Chama cha Kuhudumia
watu wenye Usonji Tanzania, Dk. Stella Rwezaula,baada ya kumaliza
mkutano na waandishi wa habari.
Mwenyekiti
wa Chama cha Kuhudumia watu wenye Usonji Tanzania, Dk. Stella Rwezaula
(kushoto), akipongezana na Mkurugenzi Mtendaji wa Lotus Clinic, Dialla
Kassam, baada ya kumaliza mkutano na waandishi wa habari.
---
Na Mwandishi Maalum
Familia nyingi Tanzania hazina ufahamu wa hali hii Na Mwandishi wetu Kliniki ya Lotus kwa kushirikiana na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, zimeanzisha kampeni mpya inayolenga kuelimisha uma kuhusu ugonjwa wa usonji (autism), ambao watanzania wengi hawaufahamu.
Familia nyingi Tanzania hazina ufahamu wa hali hii Na Mwandishi wetu Kliniki ya Lotus kwa kushirikiana na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, zimeanzisha kampeni mpya inayolenga kuelimisha uma kuhusu ugonjwa wa usonji (autism), ambao watanzania wengi hawaufahamu.
Ugomjwa huu sasa unatishia familia nyingi kwani dalili zake huanza utotoni na zinaweza kuendelea hadi ukubwani.
Akizugumza
wakati wa uzinduzi huo Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Chama cha
Kuhudumia watu wenye Usonji Tanzania, Dk. Stella Rwezaula ambaye pia ni
mtaalamu wa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na pia ana mtoto
mwenye ugonjwa huo, aliishukuru Kliniki ya Lotus kwa
kuwa katika mstari wa mbele kuanzisha kampeni hiyo ili kuwaelimisha watanzania kuhusu ugonjwa huo.
“Ni
vyema ugonjwa huu ukigundulika mapema na kutibiwa ili aliyeathirika
aweze kupona na kuishi maisha ya kawaida hapo baadaye kulingana na
athari aliyoipata. Mtoto kuanzia miaka 0-6 anaweza kutibiwa vizuri na kusaidia kubadilisha maisha yake,” alisema.
Alisema
watoto wenye hali hii wana shida katika kuwasiliana na tabia zao ni
kurudia rudia mambo anayofanya mara kwa mara na pia watuwengi wenye
ugonjwa huu wananamna yao ya kujifunza, kusikiliza na kuitika.
“Mfano
wa hali hii ni kwamba katikahali ya kawaida, mtoto wa mwaka mmoja
hutabasamu au kuwa na furaha kila wakati, huiga mambo mbalimbali
anayoona na kufuatilia vitu anavyoviona vikisogea, lakini mtoto mwenye
ugonjwa huu hafanyi vitu hivi,”alisema.
Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa Kliniki ya Lotus, Dialla Kassam alisemamuelewa
bado ni mdogo nchini Tanzania na watoto wengi huathiriwa na kuja
kujukilana wakati hali imeshakuwa mbaya zaidi.
“Kukosa
uelewa wa hali hii ya watoto wenye mahitaji huwafanya walimu na wazazi
kudhani watoto ni watundu, wavivu au wanakera na wakati mwingine
huadhibiwa kwa sababu hiyo wakati kwamba watoto hawa wanahitaji
uangalizi wa karibu, kupendwa na kupata msaada kutoka kwa walimu na wenzao,” alisema.
Alisisitiza
umuhimu wa kuwafundisha walimu na wazazi kuhusu watoto hawa wenye
mahitaji maalumu ili waweze kuwasaidia kuishi na kukubalika katika
jamii.
Alisema
kliniki yake inahudumia watoto wenye mahitaji ya aina hii jijini Dar es
Salaam na kuwa timu yake ina wataalamu mbalimbali wanaofanya kazi
pamoja ili kutoa elimu kuhusu watoto wenye matatizo haya.
“Hii
inafanyika kwa kushirikiana na mashirika ya kimataifa kwa kutoa elimu
kwa wadau mbalimbali wakiwemo walimu na wazazi kupitia warsha,mafunzo
mbalimbali, kutafuta wafanyakazi wa kujitolea na kutoa rasilimali kwa
taasisi mbalimbali kama Shule ya Mbuyuni ya watu wenye ugonjwa huu,”
alisema.
Alisema
kliniki mbalimbali kuhusu ugonjwa huo hufanyika katika Hospitall ya
Taifa ya Muhimbili kila Alhamisi na kwamba Chama Cha Watu Wenye
Usonji-Tanzania (NAPA-T) kimekuwa kikisaidia.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269