Breaking News

Your Ad Spot

Jun 15, 2015

KINANA AANZA ZIARA MKOANI GEITA, AANZIA WILAYA YA CHATU KWA KUFUNGUA MIRADI KADHAA IKIWEMO YA UMEME, MAJI A SACCOS, MAELFU WAFURIKA KWENYE MKUTANO WAKE WA HADHARA

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wananchi waliohudhuria mkutano wake wa hadhara katika Viwanja vya Stendi katika mji mdogo wa Chato, mwanzoni mwa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa iani ya CCM na Uhai wa Chama katika mkoa wa Geita, leo
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihutubia kwenye mkutano wa hadhara wa Kinana uliofanyika kwenye viwanja vya stendi katika mji mdogo wa Chato mkoani Geita.
Mkuu wa wilaya ya Chato, Rodrick Mpogolo, akisakimia wananchi katika mkutano wa hadhara wa Kinana, leo kwenye Viwanja vya Stendi katika mji mdogo wa Chato, mkoani Geita.
 Mjumbe wa NEC, waCCM wilayani Chato, Deusdedit Katwale, akisalimia wananchi katika mkutano wahadhara wa Kinana uliofanyika leo kwenye Viwanja vya Stendi katika mji mdogo wa Chato mkoani Geita, leo
 Maelfu ya wananchi wakishangilia katika mkutano wa hadhara wa Kinana uliofayika leo kwenye Viwanja vya Stendi katika mji mdogo wa Chato mkoani Geita, leo
 Moja ya mabango yaliyopamba mkutano huo wa Kinana uliofanyika leo kwenye viwanja vya stendi katika mji mdogo wa Chato mkoani Geita leo
 Mkuu wa wilaya ya Chato, Rodrick Mpogolo akishiriki katika kikundi cha kwaya kilichotumbuiza wakati wa mkutano wa hadhara wa Kinana uliofayika leo kwenye Viwanja vya Stendi katika mji mdogo wa Chato mkoani Geita leo
 Kiongozi wa Kwaya hiyo, Mariam Joseph akionyesha hisia zake wakati akiongoza kuimba wimbo maalum wakati wa mkutani huo.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitazama kwa makini wasanii waliokuwa wakitumbuiza huku wakiwa na fisi, kwenye mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu huyo uliofanyika leo kwenye Viwanja vya Stendi katika mji mdogo wa Chato mkoani Geita
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimia wananchi wenye shauku naye, alipowasili kwenye Viwanja vya Stendi katika mji mdogo wa Chato mkoani Geita, kuhutubia mkutano wa hadhara.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa nyumbaya mganga katika Zahanati ya Kata ya Ihanga, wilayani Chato mkoani Geita leo, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama katika mkoa huo
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi baada ya kushiriki ujenzi wa zahanati hiyo leo
 Kijana akiwa amebarizi juu ua mti wakati akimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana baada ya kushiriki ujenzi wa Zahanati katika kata ya Ihanga, wilayani Chato mkoani Geita, leo.
 Wasanii wakihanikiza kwa ngoma wakati Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipowasili kushiriki ujenzi wa Zahanati katika Kata ya Ihanga, wilayani Chato mkoani Geita leo.
 Wananchi katika kitongoji cha Makurugusi wilayani Chato mkoani Geita, wakiwa wamezuia msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, kudai kitongoji hicho kipatiwe Umeme wa REA, ambao nyaya zake zimepita katika eneo hilo.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki kuvuta nyaya za umeme, kwenye mradi wa ueme vijijini unaotekelezwa katika Kata ya Mkungo, wilayaniChato mkoani Geita, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa lani ya CCM na uhai wa Chama mkoani humo, leo.
 Katibu w CCM, wilaya ya Chato akimpokea Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipokaribia kuingia katika wilaya hiyo, kuanza ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama mkoani Geita leo. Wapili kulia ni Mkuu wa mkoa wa Kagera, John Mongela akisubiri kujea nyumbani baada ya kumsindikiza Kinana mwishoni mwa ziara katika mkoa wa Kagera jana.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisubiri kuvishwa skafu na Vijana wa CCM katika  mpaokezi ya kuingia katika wilaya ya Chato mkoani Geita leo. Kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.
 Kinana akivishwa skafu na Kijana wa CCM katika mapokezi yaliyofanyika katika kataya Kasenga, wilayani Chato mkoani Geita leo
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mkuu wa wilaya ya Chato, Rodrick Mpogolo wakati wa mapokezi hayo
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwasalimia wananchi wakati wa mapokezi hayo
 
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akizindua Ofisi ya CCM Kata ya Kazunguti, mwanzoni mwa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na Uhai wa Chama katika wilaya ya Chato mkoani Geita leo.
 Katibu Mkuu wa CCM, akiingia katika ofisi hiyo
 Wazaa wakimshangilia Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinanaalipohutubia mkutano wa hadhara katika kata hiyo ya Kazunguti.
 Vijana wa Kata ya Kazunguti akihanikiza kwa ngoma Kinana alipowasili kuhutubia mkutano wa hadhara katika kata hiyo
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi katika Kijiji cha Kazunguti, Kata ya Kazunguti, wilayani Chato
 Mkuu wa wilaya ya Chato Rodrick Mpogolo akimfafanulia jambo Kinana baada ya mkutano huo wa hadhara. Kushoto ni Nape
 
 Mabango ya kuwatia moyo Kinana na Nape yakiwa yameshikwa na vijana wakati Kinana alipowasili kuzindua mradi wa maji wa Kijiji cha Mlimani, katika kata ya Chato, mkoani Geita leo
 Kina mama wakimshangilia Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipowasili kuzindua mradi huo wa maji
 Katibu Mkuu wa CCM akitazama kitufe cha kuwasha mashine ya kusukuma maji, baada ya kuzindua mradi huo wa maji katika kijiji cha Mlimani Kata ya Chato, wilayani Chato mkoani Geita
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Nape wakiwa katika picha ya pamoja na vijana waliokuwa wameshika mabango ya kuwatia moyo katika kazi wanayofanya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama.
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimtwisha ndoo ya maji Paulina Fabian baada ya kuzindua mradi wa maji katika Kata ya Chato wilayani Chato mkoani Geita leo
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimpatia hati ya mkopo, mwanachama wa SACCOS ya Mshikamano Juliana Innocent, katika wilaya ya Chato mkoaniGeita leo.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCm wilaya ya Chato, mwanzoni mwa ziara yake ya kukagua utekelezaji wailani ya CCM na uhai wa Chama katika mkoa wa Geita, leo. Picha zote na Bashir Nkoromo

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages