Baadhi
ya watu wenye ulemavu wakipita na mabango yenye ujumbe katika mitaa
mbalimbali ya Jiji la Arusha kwa maandamano kwenye maadhimisho ya Siku
yao ambayo inalenga kutoa elimu ya kupinga matendo maovu wanayofanyiwa
na watu wenye nia mbaya.(Picha na modewjiblog)
Na Mwandishi wetu, Arusha
MRATIBU
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mkurugenzi wa Shirika la
Mpango wa maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodgriguez amepongeza
Tanzania kwa kuwa mstari wa mbele kushawishi dunia siku ya kukumbuka
watu wenye ulemavu wa ngozi duniani.
Alisema
dhana ya Juni 13 ilianzia Tanzania kwa mshikamano kati ya serikali ya
Tanzania na mashirika yasiyo ya kiserikali kama Shirika la Under the
same sun (TAS).
Alisema
kutokana na bidii walizoonesha Novemba 18,2014, Baraza Kuu la Umoja wa
Mataifa lilipitisha siku hiyo kuadhimishwa duniani kote kila ifikapo
Juni 13
Akihutubia
kabla ya rais Jakaya Kikwete ambaye alikuwa mgeni rasmi kuzungumza,
Rodgriguez alisema dunia inapaswa kuangalia kwa makini maisha ya
walemavu wa ngozi na kuzuia ukatili dhidi yao.
Alisema
pamoja na haja ya kuongeza ufahamu wa watu juu ya masuala ya ualibino
na maalbino ni vyema jumuiya ya kimataifa kuhakikisha kwamba kila
mwanamke, mwanamume na mtoto wanatendewa kwa usawa na kwa heshima.
Alisema
kutokana na haja hiyo Umoja wa Mataifa umekuwa ukifanyakazi na serikali
ya Tanzania kuboresha maisha ya watu wake kwa kusaidia kuimarisha mfumo
wa mahakama, masuala ya wakimbizi na masuala ya utoaji haki.
Alisisitiza kuwa kuwapo kwa haki, usawa na utu kutahakikisha kuwapo kwa amani na usalama kwa jamii zenye ulemavu wa ngozi.
Alisema
kwa sasa kuna woga mkubwa kwa jamii ya ulemavu wa ngozi kutokana na
chuki, unyanyapaa, mashambulizi ya kutisha, mauaji na kugeuzwa kuwa
bidhaa huku wakiuuawa kwa sababu za matambiko ya kutafuta utajiri.
Mratibu
huyo alisema kwamba taifa na jamii ya binadamu wote wanatakiwa
kushirikiana katika kuzuia ukatili kwa wenye ulemavu na pia kuwasaidia
kukabilina na mazingira yao magumu hasa upatikanaji wa vifaa vya
kuwakinga na madhara ya jua.
Alitaka
pia jamii kuelimishwa kuhusu mtiririko wa vinasaba vinavyosababisha
ulemavu wa ngozi na kupambana na ubaguzi na tishio la maisha kwa kutoa
mafunzo mbalimbali.
Aidha
alisema Umoja wa Mataifa utaendelea kufanya kazi na wanachama wa
taasisi mbalimbali zisizo za kiserikali na Serikali kuimarisha haki za
binadamu .
Baadhi
ya watu wenye ulemavu wakipita na mabango yenye ujumbe katika mitaa
mbalimbali ya Jiji la Arusha kwa maandamano kwenye maadhimisho ya Siku
yao ambayo inalenga kutoa elimu ya kupinga matendo maovu wanayofanyiwa
na watu wenye nia mbaya.
Baadhi
ya watu wenye ulemavu wakipita na mabango yenye ujumbe katika mitaa
mbalimbali ya Jiji la Arusha kwa maandamano kwenye maadhimisho ya Siku
yao ambayo inalenga kutoa elimu ya kupinga matendo maovu wanayofanyiwa
na watu wenye nia mbaya.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Jakaya Kikwete akihutubia
wananchi waliohudhiria maadhimisho hayo kwenye uwanja wa Sheikh Amri
Abeid jijini Arusha.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa(UN) na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) hapa nchini, Alvaro Rodriguez
akihutubia katika Maadhimisho ya Siku ya wenye Ualbino yaliyofanyika leo
kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa(UN) na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) hapa nchini, Alvaro Rodriguez
akipongezwa na Rais Jakaya Kikwete baada ya kutoa hotuba yake katika
Maadhimisho ya Siku ya wenye Ualbino yaliyofanyika leo kwenye uwanja wa
Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Balozi
wa Canada hapa nchini, Alexandre Leveque akihutubia katika Maadhimisho
ya Siku ya wenye Ualbino yaliyofanyika leo kwenye uwanja wa Sheikh Amri
Abeid jijini Arusha.
Mwenyekiti wa wenye ulemavu wa ngozi nchini(TAS), Ernest Kimaya akitoa nasaha zake.
Naibu Waziri wa Afya, Dk.Kebwe Steven Kebwe akitoa nasaha zake.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk Jakaya Kikwete akiwapongeza
watoto wenye Ualbino wanaofadhiliwa na USAID chini ya mpango wa Tuwalee.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Jakaya Kikwete akiagana na
Balozi wa Canada hapa nchini, Alexandre Leveque baada ya maadhimisho
hayo, kulia ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa(UN) na
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) hapa
nchini, Alvaro Rodriguez na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269