Mratibu
Mkazi Mashirika ya Umoja wa Mataifa (UN) na Mwakilishili wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez ambaye
alikua mgeni rasmi katika Kongamano la upatikanaji wa fedha za ndani za
maendeleo akitoa hotuba yake kwa washiriki kutoka Halmashauri za wilaya
nchini lililofanyika jijini Arusha.
Mkuu
wa Mfuko wa Umoja wa mataifa wa Ukuzaji Mitaji (UNCDF) nchini na Meneja
wa LFI duniani, Peter Malika akizungumza wakati Kongamano hilo.
Mkurugenzi
wa Huduma(Tamisemi), Denis Bandisa akizungumza wakati Kongamano ambalo
pamoja na mambo mengine alizitaka halmashauri nchini kubuni vyanzo vya
ndani vya mapato badala ya kutegemea wafadhili.
Washiriki kutoka maeneo mbalimbali nchini na nje ya nchi wakifatilia kwa makini mada katika Kongamano hilo.
Washiriki
kutoka maeneo mbalimbali nchini na nje ya nchi wakiwa katika picha ya
pamoja, Kongamano hilo limefanyika katika hoteli ya Mount Meru jijini
Arusha.
Na Mwandishi wetu, Arusha
MFUKO
wa Umoja wa Mataifa wa Ukuzaji Mitaji (UNCDF) kwa kushirikiana na Ofisi
ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),
umeitisha kongamano la siku mbili la upatikanaji wa fedha za ndani kwa
maendeleo.
Kongamano hilo linahusisha wakurugenzi wa mamlaka za serikali za mitaa nchini Tanzania na linashirikisha watu 110.
Pamoja
na wakurugenzi hao, wapo na wawakilishi kutoka Serikali Kuu na
wawakilishi walioteuliwa kutoka serikali za mitaa za Uganda, Senegal na
Benin.
Kwa
mujibu wa taarifa ya UNCDF, nia ya kongamano hilo ni kuonesha mafanikio
ya mfumo wa ukusanyaji wa fedha za ndani kuwezesha ujenzi wa
miundombinu ya kiuchumi ya kibiashara katika nchi za Tanzania na Uganda.
Taarifa
hiyo imesema kwamba baada ya kujifunza mafanikio hayo washiriki
watajadiliana na kujipanga kwa ajili ya utekelezaji wa mfumo huo katika
nchi zao wanaokotoka ili kupiga hatua mbele katika uendelezaji wa miradi
bila kutegemea fedha za nje.
Akizungumza
wakati wa ufunguzi Katibu Mkuu Tamisemi, Jumanne Sagini alisifu kazi
inayofanywa na programu ya uwezeshaji wa fedha za ndani kwa maendeleo (
Local Finance Initiative- LFI) chini ya sekretarieti ya UNCDF kwa
ubunifu wake unaowezesha kupatikana kwa mitaji ya kuwekeza katika miradi
ya maendeleo inayofadhiliwa na serikali za mitaa.
Aidha
alielezea dhamira ya serikali ya kutumia mfumo huo ulioasisiwa na UNCDF
kwa kuufanya uwe wa kitaasisi zaidi ili kuweza kusaidia kutekeleza
mipango ya maendeleo na uwekezaji ya serikali za mitaa.
Akizungumzia
umuhimu wa kongamano hilo, Mgeni rasmi, Mratibu wa Mashirika ya Umoja
wa Mataifa nchini Alvaro Rodriguez, aliipongeza serikali ya Tanzania
kwa kufuata mfumo wa utafutaji wa fedha za ndani kwa ajili ya kukuza
uwekezaji katika miundombinu ya kibiashara inayoleta mabadiliko kwa
umma.
Rodriguez
alisema katika hotuba yake kwamba kwa kuwezesha mfumo wa UNCDF LFI
kwenye serikali za mitaa ndio jibu la uhakika la uwekezaji wenye
mafanikio endelevu kwa taifa zima.
Aidha
alisema mpango huo wa LFI ambao umekuwepo nchini kwa miaka mitatu na
kuwezesha kuleta mabadiliko katika jamii, unafaa kumilikiwa na jamii ili
kuwezesha mafanikio ya juu katika uwekezaji.
Mratibu
huyo alisema kwamba Umoja wa Mataifa kupitia UNCDF utaendelea
kufanyakazi na serikali ya Tanzania,kwa kuwa wanaamini kwamba vita dhidi
ya umaskini itafanikiwa kwa kuhamisha mitaji na kuipeleka katika ngazi
za chini kwa maendeleo ya wananchi.
Kongamano
hilo ambalo ni mwendelezo wa uwezeshaji na kubadilishana uzoefu na
elimu kwa lengo la kuwezesha miradi ya umma na binafsi inayochagiza
maendeleo kujengwa; katika siku ya kwanza ya kongamano hilo washiriki
wataoneshwa miradi iliyotekelezwa manispaa ya Busia Uganda na Kibaha
nchini Tanzania.
Manispaa
ya Busia imejenga kituo cha malori, ushuru wa forodha na maeneo ya
kufanyia biashara, wakati Kibaha wamejenga kituo cha kisasa cha mabasi
na soko.
Timu
ya wataalamu wa UNCDF watawafundisha washiriki kwa siku 2 kuhusu
miradi ya maendeleo, awamu za malipo ya fedha na mikakati ya kupata
fedha na malipo na mbinu za kupunguza hatari za kibiashara.
Akisisitiza
umuhimu wa kongamano hilo Mkuu wa UNCDF nchini na Meneja wa LFI duniani
Peter Malika alisema kwamba kongamano hilo linatoa nafasi kwa
watumishi wa serikali za mitaa na wengine kujifunza namna mpya ya kupata
mitaji kwa kutumia vyanzo vya nyumbani ili kufadhili miradi ya
miundombinu ya kiuchumi inayohitajika kwa ajili ya kutoa fursa za
ujasiriamali , biashara, uwezeshaji, ajira, kuboresha maisha ya watu,
ukusanyaji kodi na utoaji huduma.
Kongamano
hilo la siku 2 ni miongoni mwa juhudi kadha za UNCDF za kuwezesha
serikali za mitaa kufikia maendeleo endelevu na kuleta athari chanya
kwa jamii ili kuondoa umaskini.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269