Breaking News

Your Ad Spot

Jun 20, 2015

HATIMAYE VIJANA WANAOSAFIRI KWA BAISKERI KUTOKA MBEYA KUELEKEA DAR ES SALAAM WAVUKA SALAMA HIFADHI YA TAIFA YA MIKUMI.

 Hii ilikuwa tarehe 15.06.2015 ambapo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro aliwaaga rasmi vijana hao ili kuanza safari yao kutoka Mbeya kwenda Dar.
 Safari yao ikiwa imeanza na hapa mmoja wa vijana hao wakiwa safarini na hapa akonesha umahili wa utaalam wa kuchezea Baiskeri Maeneo ya Chimala
 Tarehe 17.06.2015 wanawasili Iringa na kulala Hapo kisha asubuhi wanaonana na uongozi wa Polisi Mkoani Iringa
 vijana hawa watatu wakiwa Iringa sasa wanahimiza watu kujiandikisha katika Daftari la kudumu la kupigia Kura, na hapa wanadhihirisha kuwa wao wanavyo tayari, je wewe umeijiandikisha?
 Tarehe 18.06.2015 vijana hawa wanaendelea na safari yao ya kutoka Mbeya kuelekea Dar es salaam na hapa wanaanza kushuka mlima Kitonga ambapo wanaenda kulala Mikumi.
Hapa wanapumzika maeneo ya kati kati ya Mlima Kitonga
 Sasa wanapata chakula Baada ya kumaliza kushuka mlima kitonga
Usiku wa Tarehe 18.06.2015 wakiwa Mikumi  
 Haya yalikuwa ni baadhi ya Mataili ambayo walibadilisha wakiwa mikumi
 Ni Tarehe 19.06.2015 asubuhi na mapema vijana hao wakiwa wameaka ili kuzirekebisha Baiskeli zao tayari kwa kuvuka Hifadhi ya Taifa ya Mikumi.
 Tarehe 19.06.2015 vijana hao watatu wakiwa na Baiskeri zao sasa wanajiandaa na kuanza kuvuka Hifadhi ya Taifa ya Mikumi ambapo walitembea kwa Kilometa 50
 Wakiwa ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Mikumi
 Mmoja wa vijana hao akiwa anatazama ndani ya Hifadhi kama ataona wanyama
 Wakiendelea na Safari yao
 Wakimalizia malizia safari yao ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Mikumi.
Leo Tarehe 20.06.2014 vijana hawa wanaondoka Morogoro kuendelea na safari na hapa wakiwa wameweka Hema lao Mjini Morogoro.

Vijana hawa watatu ambao ni  Wise Man Tanzania,John Mwaipaya na Alex Mahenge walioamua kusafiri kwa kuendesha Baiskeri kutoka Mbeya mjini hadi Dar es salaam kwa lengo la Kuhamasisha watu kujiandikisha katika Daftari la kudumu la kupiga kura na  Baadae wakifika Jijini Dar kwa lengo la Kumpongeza Rais Dkt. Jakaya Kikwete kwa uongozi wake Bora katika kipindi cha Miaka 10 akiwa ameshika wadhifa wa Kiongozi Mkuu wa nchi.

Vijana hao ambao wameanza safari Tarehe 15.06.2015 wakitokea Mbeya sasa wapo Morogoro wanaendelea na Safari.

Na Blogs za Mikoa

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages