Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akiongozana na Mke wa Balozi wa India nchini
Tanzania Mheshimiwa Debnath Shaw wakielekea kwenye jengo la Makumbusho
ya Indra Gandhi huko New Delhi tarehe 18.6.2015. Mama Salma yupo nchini
India akiambatana na Rais Kikwete kwenye ziara siku 4 ya kiserikali kwa
mwaliko wa serikali ya India.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akitembelea sehemu mbalimbali zilizohifadhiwa
kumbukumbu za aliyekuwa Waziri Mkuu wa India Marehemo Indra Gandhi
wakati wa uhai wake. Marehemu Idra Gandhi aliuawa kwa kupigwa risasi
tarehe 31.10.1984 akiwa kwenye viwanja vya nyumba hiyo ambayo alikuwa.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akiweka saini kwenye kitabu cha kumbukumbu ya
Marehemu Indra Gandhi wakati alipotembelea makumbusho ya waziri mkuu
huyo huko New De;lhi nchini India tarehe 18.6.2015.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akiagana na kiongozi anayesimamia Makumbusho ya
aliyekuwa Waziri Mkuu wa India Marehemu Indra Gandhi (jina lake
halikuweza kupatikana) mara baada ya kumaliza kutembelea makumbusho hayo
tarehe 18.6.2015.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akipewa taarifa mbalimbali na Bwana Rajan
Madan, Mkurugenzi wa Uzalishaji katika Kiwanda cha New Holland Fiat
Limited kuhusiana na utengenezaji wa matrekta kwenye Kiwanda hicho huko
New Delhi. Mama Salma Kikwete aliambatana na Rais Kikwete kuzuru
kiwandani hapo ili kujionea utengenezaji wa matrekta.
PICHA NA JOHN LUKUWI.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269