Wafuasi
wa CUF wakinadi picha za mgombea Urais wa Chama hicho Visiwani, Seif
Shariff Hamad katika mkutano wa hadhara wa kumtambulisha mgombea huyo
uliofanyika kwenye Viwanja vya Tibilinzi- Chake chake Pemba jana. Picha
na Said Khamis
Pemba/Dar.
Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad ameitaka CCM kujiandaa
kisaikolojia kukabidhi madaraka kwa chama chake baada ya Oktoba, akisema
katika chama chake hakutakuwa na neno “kushindwa”.
Maalim
Seif, ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, aliwataka
vijana popote walipo kujiandikisha kwa ajili ya uchaguzi ili
kujitayarisha na ushindi aliouita mkubwa.
Alitoa
kauli hiyo katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Viwanja vya
Tibirinzi, Chake Chake Pemba na kuhudhuriwa na maelfu ya wafuasi wa
chama hicho kikuu cha upinzani visiwani Zanzibar.
“Hakuna
kushindwa CUF, kwa hivyo mawazo yenu yawe na kushinda tu. Vijana, hakuna
kukaa ukasema ushamaliza kupiga kura, unakwenda kwako unasubiri
ushindi. Hakuna hilo mwaka huu, lazima mjitahidi kulinda ushindi wenu,”
alisema Maalim Seif.
Katibu
huyo wa CUF alisema wananchi wa Pemba walioko Arusha, Mwanza na sehemu
nyingine warudi kujiandikisha kwenye Daftari la Wapigakura na kuwataka
kutoacha fursa hiyo ambayo ni haki yao ya kidemokrasia.
Akitilia
mkazo suala hilo, aliyekuwa waziri wa SMZ, Mansoor Yussuf Himid alimtaka
Maalim Seif baada ya kupiga kura yake kurudi nyumbani na kuwaachia
vijana kumkabidhi ushindi wa chama hicho.
Mansoor
ambaye ni mshauri wa Maalim Seif, alisema vijana wasitarajie kuletewa
ushindi katika kisahani cha chai, washiriki kikamilifu katika kupatikana
ushindi wa chama hicho.
Mansoor
alisema hatima ya ushindi wa Zanzibar ipo mikononi mwa vijana, hivyo
wanapaswa kuhakikisha ushindi wa Zanzibar unapatikana katika ya mikono
yao.
Akihutubia
mkutano huo, Mwanasiasa Hassan Nassor Moyo alisema kazi ya Maalim Seif
na aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume kuleta umoja wa
kitaifa si jambo jipya kwa kuwa lilianzia kwa Mzee Karume ambaye
alitunga sheria kuondosha ubaguzi na kuwaweka wananchi wote wa Zanzibar
kuwa kitu kimoja.
Uchumi
Katika
hotuba yake ya takriban saa moja iliyorushwa moja kwa moja na kituo cha
televisheni cha Star TV, Maalim Seif alisema Maalim Seif alisisitiza nia
yake ya kuifanya Zanzibar kuwa na mamlaka kamili ili iondokane na
adhabu ambazo siyo stahiki kwake.
Seif alisema Wazanzibari wamekuwa wakiadhibiwa kutokana na ufisadi unaofanywa na baadhi ya viongozi wa Bara.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269