Messi akitafuta maarifa ya kuwatoka wachezaji wa Jamaica katika mchezo huoTIMU
ya taifa ya Argentina imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Jamaica
usiku wa kuamkia leo katika mchezo wa Kundi B michuano ya Copa America
inayoendelea nchini Chile.
Shukrani
kwake mfungaji wa bao hilo pekee, Gonzalo Higuain dakika ya 11 tu ya
mchezo huo na sasa Argentina inakwenda Robo Fainali.
Jamaica
ambayo haijashinda mchezo wowote katika kundi hilo, tayari imeaga
michuano hiyo. Lionel Messi aliyetimiza mechi 100 timu ya taifa, sasa
anaweza kukutana na Ecuador, Peru au Venezuela katika Robo Fainali.
Kikosi
cha Argentina kilikuwa: Romero, Rojo, Garay, Demichelis, Zabaleta,
Biglia, Pastore/Pereyra dk59, Mascherano, Higuain/Tevez dk72, Messi na
Di Maria/Lamela dk84.
Jamaica:
Miller, Hector/Taylor dk71, Morgan, Laing/Dawkins dk71, Brown/Barnes
dk78, McAnuff, Watson, Austin, Mariappa, Lawrence na McCleary
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269