Breaking News

Your Ad Spot

Jun 4, 2015

MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO LEONIDAS GAMA AKABIDHIWA MRADI WA UJENZI WA UKUMBI WA CHAKULA ULIOFADHILIWA NA TANAPA.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Leonidas Gama
akisalimiana na viongozi wa wilaya ya Rombo mara baada ya kuwasili katika shule ya sekondari Olele iliyopo kata ya Olele kwa ajili ya kukabidhi Mradi wa ujenzi wa ukumbi wa Chakula uliojengwa kwa ufadhili wa Shirika la Hifadhi za Taifa , Tanzania (TANAPA).
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama
pamoja na mkuu wa wilaya ya Rombo Lembris Kipuyo wakifurahia nyimbo iliyokuwa ikiimbwa na wanafunzi wa shule ya  sekondari ya Olele wakati alipofika kwa ajili ya uzinduizi na makabidhiano rasmi ya ukumbi wa chakula uliojengwa kwa ufadhili wa Shirika la Hifadhi za
Taifa Tanzania (TANAPA).
RC ,Gamana iongozi wengine wakiskiliza
nyimbo iliyokuwa ikiimbwa na kwaya ya shule ya sekondari Olele wilayani Rombo.
Kutokana na hali ya mvua iliyokuwepo wakati
wa makabidhiano ya ukumbi wa chakula,mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Leonidas Gama alilazimika kubadili meza kuu na wao wakaa eneo ambalo pia lilikuwa na mvua huku akisema ni vyema mvua ikawanyeshea wote pamoja na wananchi.
Jengo la Ukumbi wa Chakula lililojengwa kwa
ufadhili wa Shirika la  Hifadhi za Taifa (TANAPA) katika shule ya sekondari Olele wilayani Rombo.
Meneja Ujirani Mwema kutoka Shirika la
Hifadhi za Taifa (TANAPA) Ahmed Mbugi akitoa taarifa kuhusiana na ujenzi wa ukumbi wa Chakula katika shule ya sekondari Olele.
Baadhi ya wananchi katika kata ya Olele. 
Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Hifadhi za
Taifa Tanzania,TANAPA,Ibrahim Musa akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi mradi wa ujirani mwema wa ujenzi wa ukumbi wa Chakula katika shule ya sekondari Olele wilayani Rombo.
RC,Gama na DC,Kipuyo wakilowa kutokana na
mvua iliyokuwa ikiendelea kunyesha.
Wanafunzi katika shule ya sekondari Olele
wakifuatilia hotuba ya viongozi waliofika shuleni hapo kwa ajili ya
makabidhiano ya ukumbi wa chakula uliojengwa na
TANAPA.
Mkuu wa wilaya ya Rombo ,Lembris Kipuyo
akizungumza katika hafla hiyo.
Wakazi wa kata ya Olele.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama
akihutubia wananchi waliofika katika hafla fupi ya makabidhiano ya
ukumbi wa chakula uliojengwa katika shule ya sekondari Olele wilayani
Rombo kwa ufadhili wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania
(TANAPA)
Mkuu wa mkoa wa Kilimajaro ,Leonidas Gama
akikagua jengo hilo.
Na Dixon Busagaga wa Globu aya Jamii Kanda
ya Kaskazini.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages