Mhariri
wa Gazeti la Nipashe, Jesse Kwayu (kushoto), na waombolezaji wengine
wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa mke wa mwanahabari wa Kampuni ya
The Guardian, Thobias Mwanakatwe, Levina Genda wakati wakilipekeka
kwenye gari tayari kwa safari ya kwenda Karatu mkoani Arusha kwa mazishi
yatakayofanyika kesho.
Mwanahabari
wa Kampuni ya The Guardin Ltd, Thobias Mwanakatwe akitoa heshima za
mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa mke wake, Levina Genda wakati wa
ibada ya kumuaga iliyofanyika Hospatali ya Amana Dar es Salaam leo a.
Mke wa Mwanakatwe alifariki kwa kugongwa na gari maeneo ya Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere mwishoni mwa wiki.
Waombolezaji wakiwa kwenye ibada ya kumuaga Levina Genda, iliyofanyika Hospitali ya Amana Ilala Dar es Salaam leo asubuhi.
Hapa ni huzuni umetawala.
Wafanyakazi wenzake na Thobias Mwanakatwe wa Kampuni ya The Guardian wakiwa wamejiinamia kwa huzuni.
Thobias Mwanakatwe (katikati), akiwa na wafanyakazi wenzake waliofika kumfariji.
Baadhi ya wafanyakazi wa Levina na waombolezaji wengine wakiwa kwenye ibada ya kumuaga mpendwa wao.
Kiongozi wa dini kutoka kanisa la Katoliki akiongoza ibada ya kumuombea marehemu.
Ibada ikiendelea.
Mwakilishi
wa wanahabari kutoka mkoani Mbeya ambako Mwanakatwe alikuwa
akifanyakazi kabla ya kuhamia Dar es Salaam, Patrick Kosima akitoa
akizungumza katika ibada hiyo kabla ya kutoa rambirambi ya sh.220,000.
Mhariri
wa Gazeti la Nipashe, Jesse Kwayu (katikati), akizungumza katika ibada
hiyo wakati akiwasilisha salamu za rambirambi za Kampuni ya The
Guardian.
Mdau Fabiola Bula wa Karatu, akitoa heshima za mwisho kwa marehemu.
Heshima za mwisho kwa marehemu zikiendelea.
Wafanyakazi wa Kampuni ya The Guardian wakitoa heshima za mwisho kwa wifi yao, Levina Genda. 'Hakika ni huzuni tupu'
Jeneza likiingizwa kwenye gari tayari kwa safari ya kwenda Karatu kwa mazishi.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269