Elias Nawera |
Na Dotto Mwaibale
MWENYEKITI
wa Chama cha Walaji na Tiba Tanzania , Elias Nawera, ameitaka Wizara ya
Afya na Ustawi wa Jamii kutatua changamoto ya bei kubwa ya dawa za
binadamu wanayotozwa Watanzania.
Nawera
alisema sera ya afya inasema kila mtu ana haki ya kupata huduma za afya
kwa bei nafuu, lakini bado Watanzania wengi wanakabiliwa na changamoto
kubwa ya kununua dawa kwa bei kubwa.
“Tunaomba Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii aingilie kati suala hili,
wanaoteseka kwa kiwango kikubwa ni watu wa kipato cha chini.
Nimesema hivi baada ya Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) na Baraza la Famasia kushindwa kulitafutia ufumbuzi suala hili.
Alitoa
kauli hiyo Dar es Salaam juzi, wakati akizungumza na wanahabari, ambapo
alifafanua kuwa, amefikia hatua hiyo baada ya kubaini mzigo mkubwa wa
gharama za matibabu wanaobebeshwa Watanzania.
Aidha,
Mwera alisema kupanda kwa gharama za dawa hakuna uhusiano wowote na
kupanda kwa gharama za maisha na kwamba, wizara husika ikifuatilia
inaweza kulipatia ufumbuzi suala hilo.(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269