MWILI wa
Mufti ,Alhaj Sheikh Shaban Issa Bin Simba kusafirishwa leo
Jumanne Juni 16, kuelekea mkoani Shinyanga kwa ajili ya
taratibu za mazishi.
Akizungumza
na waandishi wa habari kwenye Makao Makuu ya Baraza Kuu la Waislam
Tanzania (Bakwata), Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaj Mussa Salum,
amesema mwili wa marehemu utaswaliwa (leo) katika Msikiti wa
Msilimu, viongozi mbalimbali wa dini na serikali watakuwepo.
Amesema marehemu amefikwa na umauti huo, baada ya kusumbuliwa sana na sukari,Shinikizo la Damu (BP) pamoja na Figo.
Hata hivyo amesema kuwa juzi (Jumapili) Mufti alifanyiwa oparesheni ya figo katika Hospitali ya TMJ Jijini Dar es Salaam.
Salum amesema marehem anatarajiwa kuzikwa leo jumanne majira ya saa kumi arlasiri mkoani mkoani Shinyanga .
Sehemu
ya wanawake waliofika nyumbani kwa Marehemu Mufti Alhaj Sheikh Shabaan
Issa Bin Simba Mikocheni B jijini Dar es Salaam .
Sheikh
Mkoa wa Dar es Salaam,Alhaj Sheikh Alhad Mussa Salum akibadilishana
mawazo na Sheikh wa Mkoa wa Kigoma Hassan Kiburwa walipofika nyumbani
kwa Marehemu Mufti ,Mikocheni B jijini Dar es Salaam
Kulia
ni Sheikh wa Mkowa Dar es Salaam,Alhaj Sheikh Alhad Mussa Salum akiwa
na baadhi ya Masheikh waliofika Nyumbani kwa Marehen Mufti,Shabaan Issa
Bin Simba Mikocheni B Jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269