Breaking News

Your Ad Spot

Jun 4, 2015

SHUGHULI YA KUAGA MWILI WA MH. EUGEN MWAIPOSA ILIVYOFANYIKA JANA DODOMA KWA ALIYEKUWA MBUNGE WA UKONGA

Shughuli ya kuaga mwili wa Mhe. Eugen Mwaiposa aliyekuwa Mbunge wa Ukonga

6
Mwili wa marehemu  Mhe. Eugen Mwaiposa aliyekuwa mbunge wa Ukonga ukiwasili kwenye viwanja vya bunge  mjini Dodoma kwa ajili ya kuagwa.
11
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mhe. Martha Mlata akiimba kwa hisia wimbo wa maombolezo kwenye  shughuli ya kuaga mwili wa marehemu  Mhe. Eugen Mwaiposa aliyekuwa mbunge wa Ukonga iliyofanyika  katika viwanja vya bunge mjini Dodoma.
10
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akitoa salam za bunge  kwenye  shughuli ya kuaga mwili wa marehemu  Mhe. Eugen Mwaiposa aliyekuwa mbunge wa Ukonga iliyofanyika  katika viwanja vya bunge mjini Dodoma.
14
Mchungaji Mshana Samweli wa KKKT Jimbo la Dodoma akitoa neno kwenye shughuli ya kuaga mwili wa marehemu  Mhe. Eugen Mwaiposa leo mjini Dodoma.
12
Wabunge Mhe. Anna Abdalla (kushoto) na Mhe. Ester Bulaya wakiaga mwili wa  marehemu Mhe. Eugen Mwaiposa aliyekuwa mbunge wa Ukonga kwenye viwanja vya bunge  mjini Dodoma.
4
Mwenyekiti wa Chama cha Wabunge Wanawake Mhe. Anna Abdallah akimfariji mume wa marehemu Mhe. Eugen Mwaiposa mbunge wa Ukonga aliyefariki usiku wa kuamkia Juni 2 nyumbani kwake mjini Dodoma.
13
Baadhi ya wabunge wakitoa pole kwa wanafamilia wa marehemu Mhe. Eugen Mwaiposa aliyekuwa mbunge wa Ukonga kwenye viwanja vya bunge  mjini Dodoma.
9
Kutoka kushoto ni  Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Ombeni Sefue, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai, Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda, Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lissu, Mbunge wa Monduli Mhe. Edward Lowassa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bibi Chiku Galawa wakiwa kwenye shughuli ya kuaga mwili wa marehemu  Mhe. Eugen Mwaiposa.
7
Baadhi ya Wabunge wakiwa kwenye hali ya majonzi mara baada ya kuwasili kwa mwili wa marehemu  Mhe. Eugen Mwaiposa aliyekuwa mbunge wa Ukonga kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma .
5
Waheshimiwa Wabunge na baadhi ya watu mbalimbali waliofika kwenye viwanja vya bunge  mjini Dodoma kwa ajili ya kuaga mwili wa marehemu  Mhe. Eugen Mwaiposa aliyekuwa mbunge wa Ukonga.
2
Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lissu (kulia) akizungumza jambo na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai  mjini Dodoma kwenye shughuli ya kuaga mwili wa marehemu Mhe. Eugen Mwaiposa aliyekuwa mbunge wa Ukonga jijini  Dar es Salaam.
8
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Mhe. Edward Lowassa (kulia) akizungumza jambo na Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lissu kwenye viwanja vya bunge leo mjini Dodoma wakati wa  shughuli ya kuaga mwili wa marehemu  Mhe. Eugen Mwaiposa.
3
Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Ombeni Sefue akisaini kitabu cha wageni waliofika kwenye   shughuli ya kuaga mwili wa marehemu  Mhe. Eugen Mwaiposa aliyekuwa mbunge wa Ukonga iliyofanyika  katika viwanja vya bunge mjini Dodoma.
1
Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Ombeni Sefue (kulia) akisalimiana na Waziri wa Fedha wa zamani na Mbunge wa Kilosa Mhe. Mustafa Mkulo  alipowasili kwenye viwanja vya bunge  mjini Dodoma kwa ajili ya kuaga mwili wa marehemu  Mhe. Eugen Mwaiposa aliyekuwa mbunge wa Ukonga jijini  Dar es Salaam.(PICHA ZOTE NA FATMA SALUM – MAELEZO).

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages