Balozi
wa Spain nchini, Mh. Luis Cuesta Civis (kushoto) na Mratibu Mkazi wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la
Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (wa pili kushoto)
wakikagua mitaala ya kufundishia kwenye ofisi za walimu katika shule ya
msingi Yombo ambayo imejengwa na mradi wa awamu ya pili wa Mfuko wa
Maendeleo ya Jamii (TASAF) iliyopo katika kijiji cha Chasimba, wilayani
Bagamoyo mkoa wa Pwani, wakati wa kukagua miradi inayofadhiliwa na
TASAF wilayani humo huku Afisa Program Kitengo cha Uahulishaji Fedha
(TASAF), Edith Mackenzie (wa pili kulia) akitoa maelezo kwa ugeni
huo.(Picha na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
Na Mwandishi Wetu, Bagamoyo
MRATIBU
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Tanzania Alvaro Rodriguez
ametaka serikali za tawala za mikoa na serikali za mitaa kuwezeshwa
zaidi ili kuweza kuwatumikia wananchi.
Aliyasema
hayo wakati alipozuru kijiji cha Chasimba mwishoni mwa juma akiwa na
Balozi wa Hispania Luis Cuesta Civis kuona miradi ya maendeleo
inayofadhiliwa kwa pamoja kati ya serikali ya Tanzania, Mashirika ya
Umoja wa Mataifa na Ubalozi wa Hispania.
Mratibu
huyo alisema kwamba mafanikio makubwa yanayoonekana katika kijiji cha
Chasimba ni matokeo ya ushirikiano mzuri wa wadau wa maendeleo na
wanakijiji.
Alisema ushirikiano huo ni muhimu katika kutokomeza umaskini uliokithiri katika jamii.
Alisema
pamoja na mafanikio hayo Umoja wa Mataifa na wadau wengine wa maendeleo
wangelipenda kuona serikali za mitaa zinawezeshwa zaidi ili kuweza
kusaidia jamii kama inavyofanyika sasa katika kijiji cha Chasimba.
Kijiji
hicho ni miongoni mwa vijiji kadhaa nchini vinavyofaidika na mpango
unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii, TASAF, ambao nao
unachangiwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa na wadau wengine wa
maendeleo.
Alisema
anapenda kuona kwamba maisha ya wakazi wa kijiji hicho yanabadilika na
kuwa kama ya mama Kicheko ambaye ameondoka katika umaskini uliokithiri
baada ya kutumia vyema mradi uliofikishwa kijijini hapo.
Alitoa
wito kwa wadau wa maendeleo na mashirika ya kimataifa kusaidia
kuwezesha serikali za mitaa na mashirika yanayoapambana na umaskini
nchini kuwezesha miradi ya kuondoa umaskini kufanikiwa.
Bi.
Kicheko ambaye mwaka mmoja uliopita alikuwa hohehahe kwa sasa
anatengeneza sabuni, ameboresha nyumba yake kwa kuiwekea bati na ana
kula mlo zaidi ya mmoja sasa.
Katika
ziara hiyo, Mratibu huyo alitaka kujua wananchi wa Chasimba katika
miaka mitano hadi saba ijayo wanataka kuwaje na kujibiwa kwamba wanataka
kuwa na hali bora zaidi ilivyo sasa na kuanzisha viwanda vidogo.
Balozi
wa Spain nchini, Mh. Luis Cuesta Civis (kushoto) na Mratibu Mkazi wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la
Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia) wakipitia
baadhi ya kurasa za mwongo wa kufundishia kitabu cha Uraia wakati wa
ziara ya kukagua miradi inayofadhiliwa na TASAF wilayani Bagamoyo mkoa
wa Pwani.
Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Ladislaus
Mwamanga, alisema mpango huo wa miaka 10 ambao umeingia katika mwaka wa
tatu umelenga kuwezesha afya, elimu na lishe na sasa wanafanya
kuwajengea uwezo wa kuweka akiba na kuwekeza.
Alisema uwekaji akiba huo unawezekana kwa kutoa ajira wakati wa vipindi vigumu.
Alisema
mpango huo wa kukabili umaskini uliokithiri unachangiwa pamoja na Benki
ya Dunia, Shirika la Maendeleo la Uingereza, Shirika la maendeleo la
Sweden na serikali ya Tanzania.
Alisema kuna kaya milioni moja zinazokula mlo mmoja ambazo zinatakiwa kubadilishwa kuwa katika hali bora.
Aidha alisema wameshakamilisha kutengeneza ramani ya umaskini baada ya kumaliza kuandikisha kaya maskini zilizopo nchini.
Diwani
wa kata ya Yombo ambapo kijiji cha Chasimba aliyejitambulisha kwa jina
la Idd alisema kwamba ni matraajio yao katika miaka 10 ijayo kubadilika
kabisa kutokana na kijiji hicho kuwa na umeme na maji ya kutumia.
Alisema hata hivyo wanahitaji msukumo zaidi ili kuwa na viwanda vidogo.
Naye
balozi wa Hispania nchini, Luis Cuesta Civis alisema kwamba
amefurahishwa na matokeo ya fedha ambazo nchi yake imezitoa zipatazo
bilioni 1.3 za maendeleo ambazo nyingine zimepelekwa TASAF.
Kijiji
cha Chasimba kina kaya 197 zinazonufaika na mpango wa kunusuru kaya
maskini TASAF III (PSSN) ambapo tayari wamepewa ruzuku ya shilingi
43,227,190 katika mikupuo 9.
Imeelezwa
kuwa kumekuwepo na mafanikio makubwa tangu kuanza kwa mradi wa PSSN
kijijini hapo. Mafanikio hayo ni pamoja na kumekuwepo na ongezeko la
wanafunzi wanaoandikishwa na kuhudhuria shule, aidha madarasa matatu
yamejengwa na ofisi ya mwalimu.
Balozi
wa Spain nchini, Mh. Luis Cuesta Civis (kushoto) na Mratibu Mkazi wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la
Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (katikati) huku Afisa
Program Kitengo cha Uahulishaji Fedha (TASAF), Edith Mackenzie (kulia)
akiwapitisha kwenye baadhi ya maeneo katika mwongozo wa kitabu cha
kufundishia somo la Urai walipofanya ziara ya kukagua miradi
inayofadhiliwa na TASAF, wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
Balozi
wa Spain nchini, Mh. Luis Cuesta Civis (kushoto) na Mratibu Mkazi wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la
Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez wakiendelea na ukaguzi
katika mazingira ya shule ya msingi Yombo ambayo imejengwa na mradi wa
awamu ya pili wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) iliyopo katika
kijiji cha Chasimba, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani, wakati wa kukagua
miradi inayofadhiliwa na TASAF wilayani humo.
Wanafunzi
wa shule ya msingi Yombo ambayo imejengwa na mradi wa awamu ya pili wa
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) iliyopo katika kijiji cha Chasimba,
wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani, wakiwakaribisha wageni (hawapo pichani)
waliotembelea shule yao wakati wa kukagua miradi inayofadhiliwa na
TASAF wilayani humo.
Balozi
wa Spain nchini, Mh. Luis Cuesta Civis (wa pili kushoto) na Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez (wa pili kulia)
wakimsikiliza Mwanafunzi wa darasa la saba Nadhifa Harubu (katikati) wa
shule ya msingi Yombo ambayo imejengwa na mradi wa awamu ya pili wa
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) iliyopo katika kijiji cha Chasimba,
wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani, wakati wa kukagua miradi
inayofadhiliwa na TASAF wilayani humo. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Ladislaus Mwamanga na Kushoto ni
Mkurugenzi wa Miradi wa TASAF, Amadeus Kamagenge.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez (kulia) akipitia
daftari la Mwanafunzi wa darasa la saba Nadhifa Harubu (katikati) wa
shule ya msingi Yombo ambayo imejengwa na mradi Mfuko wa Maendeleo ya
Jamii (TASAF) kupitia awamu ya pili ya mradi wa TASAF iliyopo katika
kijiji cha Chasimba, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani, wakati wa kukagua
miradi inayofadhiliwa na TASAF wilayani humo, huku Balozi wa Spain
nchini, Mh. Luis Cuesta Civis (kushoto) akifurahi jambo wakati wa ziara
hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Ladislaus
Mwamanga (kushoto) akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi
Yombo wakati wa ziara ya Balozi wa Spain na Mratibu Mkazi wa Umoja wa
Mataifa walipotembelea wilayani Bagamoyo kukagua miradi inayofadhiliwa
na TASAF.
Bi.
Kicheko Omary (kushoto) mkazi wa kijiji cha Chasimba kata ya Yombo
anayenufaika na mradi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika
Mpango Kunusuru Kaya Maskini (PSSN) akielezea mafanikio aliyoyapata
tangu alioanza kupokea ruzuku za TASAF.
Balozi
wa Spain nchini, Mh. Luis Cuesta Civis (wa pili kushoto) na Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez (wa pili kulia)
wakiangalia zao la Mihogo inayolimwa na Bi. Kicheko Omary (kushoto)
mkazi wa kijiji cha Chasimba kata ya Yombo anayenufaika na mradi wa
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika Mpango Kunusuru Kaya Maskini
(PSSN) ambapo Mama huyo ameweza kuboresha nyumba yake kwa kununua Bati,
Sementi, kuweka Umeme wa jua (Solar Power), kuvuta bomba la maji, Kilimo
cha Mihogo, Nazi, Miwa na Mboga mboga wakati wa ziara ya siku moja
kukagua miradi inayofadhiliwa na TASAF wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
Kulia ni Afisa Program Kitengo cha Uahulishaji Fedha (TASAF), Edith
Mackenzie. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa
Maendeleo ya Jamii (TASAF), Ladislaus Mwamanga na Mkurugenzi wa Miradi
wa TASAF, Amadeus Kamagenge (wa pili kulia) Wengine katika picha ni
wajukuu wa Bi. Omary, Grace Gemini (6) na Mariamu Gemini (10).
Balozi
wa Spain nchini, Mh. Luis Cuesta Civis na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya
Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa
Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez katika picha ya pamoja na familia ya
Bi. Kicheko Omary.
Balozi
wa Spain nchini, Mh. Luis Cuesta Civis (katikati) na Mratibu Mkazi wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la
Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez (kushoto) wakiangalia zao la
mboga ya Kisamvu walipotembelea shamba la Bi. Twajuana Mohamed (kulia)
anayenufaika na mradi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika
Mpango Kunusuru Kaya Maskini (PSSN) ambapo ameweza kufuga Kuku wa
kienyeji, kujenga choo cha kisasa, Kilimo pamoja na kukunua mabati ya
kuezekea nyumba yake kupitia mradi huo wakati wa ziara ya siku moja
katika kijiji cha Chasimba, kata ya Yombo wilayani Bagamoyo mkoani
Pwani.
Bi. Twajuana Mohamed (kushoto) akiwa ameongozana na Mratibu Mkazi wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la
Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia) pamoja na
Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Ladislaus
Mwamanga kukagua shamba la Bi. Mohamed ambaye amenufaika na mradi wa
TASAF katika kujikwamua kiuchumi. Wa pili kulia ni Afisa Program Kitengo
cha Uahulishaji Fedha (TASAF), Edith Mackenzie.
Bi.
Twajuana Mohamed ambaye ananufaika na mradi wa Mfuko wa Maendeleo ya
Jamii (TASAF) katika Mpango Kunusuru Kaya Maskini (PSSN) akionyesha
ugeni huo choo alichojenga baada ya kunufaika na mradi huo.
Balozi
wa Spain nchini, Mh. Luis Cuesta Civis na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya
Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa
Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko
wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Ladislaus Mwamanga kwenye picha ya pamoja
na familia ya Bi. Twajuana Mohamed ambaye ananufaika na mradi wa Mfuko
wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika Mpango Kunusuru Kaya Maskini (PSSN)
sambamba na wajukuu zake.
.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269