Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (pichani) ,
amenusurika kifo baada ya ndege aliyokuwa akisafiria kutoka Iringa
kwenda Zanzibar kutaka kugongana uso kwa uso na ndege nyingine dakika
moja kabla ya kutua.
Waziri
Membe akiwa na ujumbe wake wa watu wanane, walikuwa wakisafiria ndege
ya kukodi kampuni ya 5H NEG Precition Aviation ikirushwa na rubani
Mathew Mhahiki, ambaye ameonyesha kushangazwa na tukio hilo alilodai “ni
kwa rehema za Mungu tumepona ajali hii.”
Akizungumza
na mwandishi wetu aliyeko katika ziara yake, rubani Mhahiki alisema:
“Lazima kuna tatizo katika control center hata hivyo tayari nimeongea
nao na wameniomba samahani na kudai walipitiwa, maana kwa hali
ilivyokuwa ni kwamba tungegongana wakati wa kutua maana nimeshangaa tu
kuona ndege hii hapa ndiyo maana nikaamua kumkwepa mwenzangu nikapanda
juu.”
Waziri
Membe alisema: “Nina uzoefu mkubwa wa kusafiri na ndege mahali pengi
duniani, hali hii ilikuwa ni ajali na labda sasa tungekuwa dead bodies,
lakini ninajua Mungu yuko upande wetu katika safari hii ya uhakika,
lakini pia izingatiwe nimekuja kufanya kazi ya Mungu.”
“Katika
safari hii tutashuhudia mambo mengi sana, lakini kwa kuwa kila
ninapotaka kuondoka nyumbani ama hotelini mara nyingi nimekuwa
nikimtanguliza Mungu maana bila Mungu hii ilikuwa ni mwisho wa maisha
yetu tuliokuwa kwenye ndege hii.”
Waziri
Membe alikuwa amealikwa mjini hapa na Umoja wa Akimama wa Kikristu
(Umaki) wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Zanzibar waliokuwa wakifanya
mkutano wao mkuu unaofanyika kila baada ya miaka mitano akitokea Iringa
ambako alikwenda kutafuta udhamini wa chama ili kumwezesha kugombea
urais kupitia Chama Cha Mapinduzi, CCM.
Akiwa
uwanjani hapo, Waziri Membe alikutana na Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu
Nchemba aliyekuja hapa Zanzibar kutafuta wadhamini ambapo makada hao
walipata nafasi ya kuzungumza.
Akiwa
katika mkutano huo, Waziri Membe alisema: "Miongoni mwa mambo
yanayonikera ndani nafsi yangu ni kuona mwanamke bado anaachwa nyuma,
hili halipendezi, ni lazima tuhakikishe wanawake wanapata elimu ya
ufundi stadi maana mwanamke akiwezeshwa hasa katika eneo hili la elimu
wanaweza hata kushinda wanaume wengi.”
“Ni
lazima kina mama wawezeshwe kujiajiri ili msiwategemee kina baba kwa
kila jambo lakini pia ili kufikia malengo hayo ni lazima tuwape elimu
kina mama.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269