.

BANZASTONE AZIKWA LEO JIJINI DAR ES SALAAM

Jul 18, 2015


 theNkoromo Blog
Mwanamuziki maafuru hapa nchini Tanzania, Ramadhani Masanja, aliyetamba zaidi kwa jina la Banzastone, (kulia), leo amezikwa jijini Dar es Salaam, baada ya kufariki jana, nyumbani kwao, Dar es Salaam, baada ya kuungua kwa mda mrefu.

Mazishi ya Masanja ambaye alizaliwa mwaka 1972 yamehudhuriwa wasanii mbalimbali akiwemo Tumaini ambaye Baada ya Kapteni John Komba aliyefariki mapema mwaka huu, ndiye Mkurugenzi wa TOT Plus, bendi ambayo alitamba nayo sana baada ya kujiunga na bendi hiyo akitokea bendi ya African Stars, Wana Twanga Pepeta inayomilikiwa na mwanamama Asha Baraka.

Banzastone anakumbukwa kwa nyimbo nyingi zenye busara alizoimba, ukiwemo wa Mtaji wa Masikini ni nguvu zake mwenyewe alioimba akiwa na TOT Plus kama kiongozi wa bendi.
   Banzastone alisoma katika shule ya msingi Mnazi Mmoja alikomaliza shule mwaka 1987, lakini hakuendelea na masomo zaidi kutokana na kupenda sanaa ya muziki.

Katika harakati zake za kupenda muziki wazazi wazazi wake walipinga, hata hivyo miaka ya 1990 alijikita katika kucheza dansi kwenye sherehe za harusi na kwenye mashindano mbalimbali ya muziki wa disko kabla ya kuanza muziki wa dansi katika bendi nilizotaja hapo awali.

 Waombolezaji wakiwa makaburini kumzika banzastone leo
 Mkongwe wa muziki wa dansi hapa nchini, Juma Mapili (kushoto) akiwa makaburini wakati wa mazishi hayo
 Tumaini wa TOT Plus (kulia) akiwa makaburini kwenye mazishi hayo
Wasanii na wanamuziki mbalimbali wakiwa makaburini wakati wa mazishi hayo. Picha na mitamdao na imetayarishwa na theNkoromo Blog

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª