.

JUMUIYA YA WATANZANIA WA DMV NA WASHIRIKA WAO WATOA HUDUMA ZA KIMATIBABU NA MADAWA BURE KATIKA HOSPITALI YA MWANAYAMALA JIJINI DAR

Jul 22, 2015

Mkurugenzi wa Taasisi ya kinamama wa Kiafika inayohusika na ugonjwa wa Saratani ya matiti Bi. Ify Nwabuku(kushoto) akizungumza na wakina mama (hawapo picha) wakati wa utoaji wa matibabu bure kwa wakina mama katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar. Kushoto ni Bi Asha Nyang'anyi ambaye ni mwanakamati wa ustawi wa jamii na maendeleo ya kiuchumiwa jumuiya ya Watanzania DMV.
 Wakina mama wakimsikiliza kwa makini Bi. Ify Nwabuku wakati akitoa maelezo juu ya upimaji wa Saratani kwa wakina mama waliofika kupima afya zao katika hospitali ya Mwananyamala zilizokuwa zikitolewa na Jumuiya ya Watanzania DMV pamoja na  washirika wao walioamua kutoa huduma za kitabibu na madawa bure.
 Dk. George Quintero(kushoto) kutoka Marekani akimtibu meno mtoto Living Andrew aliyeshikwa na mama yake huku akisaidiana na Dk. Emilton Ndashau(kulia) wakatia wa utoaji wa uduma bure iliyodhaminiwa na Jumuiya ya Watanzania DMV pamoja na  washirika wao katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar.
 Dk. Somtochukwa Agunwah(kushoto) kutoka Marekani akimtibu mmoja wa mama aliyekuwa anaumwa jino katika hospitali ya Mwananyamala huku akisaidiwa na Dk. Kilechi Nwankwo(kilia) kutoka Marekani pamoja na Dk. Kisumo Armogaston.
 Dk. William Desdery ambaye ni daktari wa macho akimtibu mmoja wa wakina mama waliofika katika hospitali ya Mwananyamala jijini dar kwa ajili ya matibabu yanayotolewa bure na Jumuiya ya Watanzania DMV pamoja na  washirika wao.
Dk. Sharon Sagoo akipima dawa zilizotolewa na Jumuiya ya Watanzania DMV pamoja na  washirika wao  kwa ajili ya kupewa mgojwa waliokuwa wanaumwa katika hospitali ya Mwananyamala 
 
 Dk. Jummy Amuwo akihakiki madawa
 Hizi ni baadhi ya Dawa zilizotolewa na Jumuiya ya Watanzania DMV pamoja na  washirika wao kwa ajili ya wagonjwa wa Hospitali ya Mwananyamala na pia zinatolewa bure.
Rais wa Jumuiya ya Jumuiya ya Watanzania DMV, Bw. Iddi Sandaly(kustoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Bi. Adama Gibateh(katikati) pamoja na Kushoto ni Bi Asha Nyang'anyi ambaye ni mwanakamatiwa ustawi wa jamii na maendeleo ya kiuchumiwa jumuiya ya Watanzania DMV.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช