Dk. Ally Y. Simba
Waziri wa
Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa hivi
karibuni alimteua Dk. Ally Yahaya Simba kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka
ya Mawasiliano Tanzania, (TCRA) kufuatia mchakato wa kumpata Mkurugenzi
Mkuu kama ilivyoainishwa katika Sheria ya Kuanzishwa kwa Mamlaka ya
Mawasiliano ya 2003 kifungu cha 9 na kifungu cha 13. (TCRA Act, 2003)
Dk. Simba
aliteuliwa rasmi kushika wadhifa huo mnamo tarehe 6 Jula1 2015 kwa
kipindi cha miaka mitano. Kabla ya uteuzi huo, Dk. Simba alikuwa Kaimu
Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) Wizara ya
Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia tangu Agosti 2013.
Dk. Simba
ana uzoefu wa zaidi ya miaka 16 katika Sekta ya Mawasiliano ambapo
amefanya kazi kwa watoa huduma, Taaluma ya Utafiti, Udhibiti pamoja na
Serikali Kuu.(P.T)
Dk. Simba
ana Shahada ya B.Sc. (Hons.) Shahada ya Sayansi ya Elektroniki na
Mawasiliano kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Tanzania, aliyopata
mwaka 1998. Pia ana Shahada ya Uzamili ya Uhandisi aliyoipata mwaka 2003
na Shahada ya Uzamivu (Ph.D) ya Uhandisi wa Kielektroniki kutoka Chuo
Kikuu Cha Hokkaido, Sapporo, nchini Japan, aliyoipata mwaka 2006.
Kuanzia
mwaka 2006 mpaka 2011, Alikuwa Mtaalamu Mtafiti katika Taasisi ya Taifa
ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, huko Tokyo, Japan, ambako
alihusika katika kufanya utafiti wa madhara ya ya kiafya kwa mwanadamu
kwa kutumia simu za mikononi na kwa kuwa karibu na minara ya
mawasiliano.
Mnamo
mwaka 2011 hadi mwaka 2013, alifanya kazi Mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania (TCRA) kama Meneja Mipango na Utafiti wa Mamlaka.
Dk. Simba
ametoa machapisho kadhaa yaliyosambazwa kote duniani katika majarida ya
kimataifa na amewasilisha matokeo ya tafiti zake katika zaidi ya
mikutano 30 ya kimataifa ndani na nje ya Tanzania. Aidha Dk. Simba
alikuwa Kiongozi wa timu ya wataalamu wa Kitanzania iliyoandaa Sheria za
Uhalifu wa Mitandao nchini iliyopitishwa na Bunge hivi karibuni.
Dk. Simba
ni Mhandishi Mahiri (Chartered Engineer), aliyesajiliwa nchini
Uingereza katika Baraza la Uhandisi nchini humo na ni “Fellow” wa
Taasisi ya Uhandisi na Teknolojia ya nchini Uingereza, ambako alifanya
kazi kama Mshauri wa Kimataifa wa Usajili wa Wanataaluma Wahandisi
kutoka Aprili 2011 mpaka Machi 2014.
Pia Dk.
Simba ni Mwanachama wa “Institute of Electrical and Electronics
Engineers” (IEEE). Hali kadhalika Dk. Simba amechapishwa katika jarida
la “Marquis Who's Who in Science and Engineering” katika toleo la 11, la
mwaka 2011–2012.
Dk. Simba ni miongoni waliopata Udhamini wa Serikali ya Japan (Monbukagakusho Scholarship) kutoka mwaka 2000 mpaka 2006.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269