.

KIKWETE APOKEA HUNDI YA BIMA YA MAISHA

Jul 21, 2015


mail.google.com
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea hundi ya malipo ya Bima ya Maisha(Flexi Provider) kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Bima la Taifa(National Insurance Corporation of Tanzania Limited) NIC Bwana Sam Kamanga ikulu jijini Dar es Salaam julai 21, 2015.
B
Akimkabidhi hundi hiyo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima Tanzania Limited (NIC) Bw. Sam Kamanga amesema uwepo wa Mheshimiwa Rais kama mteja wa NIC imesaidia kukuza uelewa na shughuli za shirika hilo.
“Kitendo cha Serikali kukatia Bima mali zake na taasisi zake, kumeongeza uwezo wa kifedha wa shirika na soko la Bima” amesema na kuwataka watu binafsi, taasisi mbalimbali na mashirika ya kiserikali kukata Bima kwa ajili ya maendeleo na akiba ya baadaye.
Rais Kikwete ameitaka NIC kuongeza juhudi katika kuhamasisha na kuelimisha watanzania umuhimu na manufaa makubwa yanayopatikana kutokana na Bima

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช