.

RAIS KIKWETE AKABIDHIWA JOHO NA CHETI CHA SHAHADA YA DOCTOR OF LAWS

Jul 21, 2015

JK1
Makamu Mkuu wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza Mukandala akimkabidhi Rais Dkt . Kikwete cheti cha Shahada ya Heshima ya Doctor of Laws (Honoris Causa) wakati wa hafla fupi ya kumkabidhi Rais joho na cheti iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na maprofesa waandamizi wa chuo hicho.Tayari Rais Kikwete alishatunukiwa shahada hiyo katika mahafali ya 41 ya UDSM yaliyofanyika Octoba mwaka 2011.
JK4
Profesa Agnes Mwakaje wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akimvika kofia ya kitaaluma Rais Dkt. Kikwete wakati wa hafla fupi ya kumkabidhi Rasmi Rais Joho na cheti cha shahada ya heshima ya Doctor  of Laws (Honoris Causa) ikulu jijini Dar es Salaam.
JK6
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza Mukandala akisoma maelezo mafupi baada yeye na jopo la maprofesa waandamizi wa chuo hicho kumkabidhi Joho la taaluma na cheti cha Shahada ya heshima ya Doctor of Laws (Honoris Causa) ya chu kikuu cha Dar es Salaam wakati wa hafla iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam
JK7
Rais Dkt. Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza Mukandakla pamoja na maprofesa waandamizi wa chuo hicho muda mfupi baada hafla fupi ya kumkabidhi Rais Joho na Cheti cha Shahada ya Heshima ya Doctor of Laws (Honoris Causa) ikliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo (picha na Freddy Maro)

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช