Meneja
Uhusiano na Mawasiliano wa Taasisi ya Maendeleo ya Elimu Mkoa wa
Morogoro (MEDO), James Mbuligwe (kushoto), akizungumza katika mkutano na
waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kabla ya MC Pilipili kutiliana
saini na taasisi hiyo ya kusaidia elimu. Kutoka kulia ni Meneja Mradi,
Bertha Gama, Emmanuel Elias 'MC' Pilipili na Makamu Mwenyekiti wa Medo,
Seluwa Amin.
MC Pilipili (katikati), akizungumza kabla ya kutia saini.
Makamu Mwenyekiti wa Medo, Seluwa Amin (kushoto), akiangalia mkataba huo kabla ya kusainiwa.
MC Pili pili (katikati), akisaini mkataba huo.
Makamu Mwenyekiti wa Medo, Seluwa Amin (kushoto), akimkabidhi mkataba huo MC Pilipili. Kulia ni Meneja Mradi Medo, Bertha Gama.
Na Dotto Mwaibale
MSANII
na mshereheshaji wa shughuli mbali mbali, Emmanuel Elias 'MC' Pili pili
ameingia mkataba na Taasisi ya Maendeleo ya Elimu Mkoa wa Morogoro
(Medo), kwa ajili ya kusaidia elimu.
Akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kabla ya kusaini mkataba wa
kusaidia watoto walio katika mradi wa elimu kwa watoto unaoendeshwa na
Medo, Pilipili alisema ni wakati muafaka kwa watanzania kwa ujumla
kujenga tabia ya kusaidia shughuli za maendeleo hasa katika elimu.
Alisema
bila ya kuwa na elimu hakuna kinachoweza kufanyika katika mambo
mbalimbali pamoja na uongozi hivyo kila mtu eneo alipo anapaswa kusaidia
elimu kupitia taasisi hiyo ya Medo ili iweze kuwasaidia watoto wengi
zaidi.
"Napenda kuwasapoti watoto hawa waliochini ya mradi
unaoendeshwa
na Medo kwa kuwasaidia mahitaji mbalimbali hivyo naomba watanzania
wanisapoti wakiwemaniio wasanii wenzangu" alisema Pilipili.
Meneja
Uhusiano na Mawasiliano wa Taasisi ya Maendeleo ya Elimu Mkoa wa
Morogoro, James Mbuligwe alisema taasisi yake kuingia mkataba na MC Pili
pili kwa ajili ya kuwasaidia watoto hao ni hatua nzuri ya mafanikio
kwao.
Alisema
taasisi hiyo imezindua kampeni maalumu ya 'Nisaidie 500 Yatosha kunipa
elimu ambapo balozi wa mradi huo ni Msanii Wastara Sajuki" alisema
Mbuligwe.
Meneja
wa Mradi huo, Bertha Gama alisema hadi hivi sasa kuna watoto 35
wanaopata elimu ya Sekondari katika shule za Kauzeni, Kihonda,
Mwembesongwe na Mzinga na kuwa mwaka huu wanafunzi wanne waliochini ya
mradi huo wanategemewa kuhitimu kidato cha nne.
Alisema
lengo la taasisi hiyo ni kufikisha huduma zao nchi nzima ambapo kwa
awamu ya kwanza wameanzia mkoani Morogoro na kupitia chini ya mradi huo
watoto 100 watanufaika na kwa awamu ya pili wanatarajia kuifanya mikoa
ya Kanda ya Ziwa. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269