MKUU
wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (pichani), ameahidi kusomesha
watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu 12, ikiwa ni
kuwalipia ada za shule.
Hayo
aliyabainisha Dar es Salaam jana wakati Kampuni ya Simu za mkononi
Zantel ikikabidhi kisima cha maji safi katika kituo cha kulea watoto
yatima na wanaoishi katika mazingira magumu cha Watoto Wetu Tanzania
kilichopo Mbezi Suka jijini Dar es Salaam.
Watoto
hao 12, ambapo 8 kati yao wana elimu ngazi ya sekondari huku 3
wakitakiwa kwenda chuo kikuu na 1 kuahidiwa endapo atafaulu kidato cha
nne sanjari na kuongea na mifuko ya hifadhi za jamii kuona jinsi gani
wanaweza kusaidia kundi hilo katika huduma za afya.
Makonda
alisema familia ni chanzo cha kuongeza idadi ya watoto wanaoishi katika
mazingira magumu kutokana na ugumu wa maisha, kuoana katika umri mdogo
na uelewa mdogo wa maana ya familia.
"Familia
ni chanzo kizuri cha kuongeza au kupunguza idadi ya watoto wa mitaani,
familia nyingi hazina uvumilinu ndani ya ndoa zao...msijitazame kama
yatima kwasababu hamtaweza kuwa na maendeleo mazuri,"alisema Makonda.
Kwaupande
wake Mkurugenzi mtendaji Kampuni ya Zantel, Pratap Ghose alisema
kampuni hiyo imekuwa ikionesha jitihada za kusaidia maendeleo ya kijamii
na kiuchumi kwenye jamii inayoizunguka.
"Kampuni
yetu inalenga kugusa maisha ya wananchi wanaotuzunguka, na ndio maana
tumeamua kutoa msaada wa kisima ili kiweze kukisaidia kiyuo hiki
kumaliza moja ya matatizo yaliyokuwa yanawakabili kwa muda
mrefu,"alisema Ghose.
Mkuu
wa kituo cha Watoto Wetu Tanzania, Evance Tegete alisema awali kituo
kilikuwa kinategemea maji kutoka Dawasco ambayo upatikanaji wake ulikuwa
si wa uhakika, hivyo wanaishukuru kampuni hiyo kwa kuwachimbia kisima
hicho.
Kituo
cha Watoto Wetu tanzania kilianzishwa mwaka 2001,ambapo hadi sasa kina
watoto 70, kuanzia umri wa miaka 5 hadi 25 kutoka mikoa mbalimbali
kikiwa na lengo la kuhakikisha watoto wasio na wazazi au walezi wanapata
matunzo na elimu bora. ((Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba-0712-727062)
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269