Breaking News

Your Ad Spot

Jul 10, 2015

TANZANIA MWENYEJI WA MKUTANO MKUU WA UTUMISHI WA JUMUIYA YA MADOLA

Na Pius Yalula-MAELEZO

Tanzania inatarajia  kuwa mwenyeji wa mkutano wa 12 wa watumishi wa umma wa  nchi za Afrika ambazo ni wanachama Jumuiya ya Madola utakaonza Jumatatu ijayo jijini Dar es salaam.


Mkutano huo unatarajiwa kufunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimimwa Dokta Jakaya Mrisho Kikwete na kufungwa na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Dokta Ali Mohamed Shein


Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Katibu Mkuu , Ofisi ya Rais Menejimenti  ya Utumishi wa Umma leo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) jijini Dar es salaam.


Amesema kuwa Mkutano huo unatarajia utakaonza tarehe 13 na kumalizika tarehe 15 unatarajiwa kujumuisha nchi  18 za Afrika ambazo ni wanachama wa Jumuiya ya Madola .


Bwana Mkwizu amezitaja nchi hizo ni Botswana,Namibia,Cameroon,Ghana,Kenya,Lesotho,Malawi,Mauritius,Msumbiji,Namibia,Nigeria,Rwanda,Sychelles,Sierra Leone,Afrika Kusini,Swaziland,Tanzania,Uganda,Uganda na Zambia.


Ameongeza kuwa wakati wa mkutano huo washiriki watapata fursa ya kujadili changamoto mbalimbali zinazoukabili utumishi wa umma wa nchi husika na kubadilishana uzoefu ili kuimarisha utendaji na ufanisi katika utumishi wa umma.


Aidha Kaimu Katibu Mkuu huyo amesema kuwa wageni hao watapata fursa ya kutembelea  mji wa kihistoria wa Bagamoyo,ili kuwapa fursa  ya kujifunza hazina kubwa ya kihistoria katika mji huo.


Hivyo , ametoa wito kwa wananchi wote kuonyesha moyo wa ukarimu kwa wageni katika kipindi chote cha mkutano ili kuendeleza jina zuri la Tanzania

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages