Mtaalam
wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce
Temu akimwelekeza Mkurugenzi wa kampuni ya Events World, Dimo Debwe
Mitiki, jinsi ya kuwasilisha maoni yake kuhusiana na kazi za Umoja wa
Mataifa na nini angependa Umoja huo ufanye zaidi kwa ajili ya watanzania
kwenye viwanja vya maonyesho ya 39 ya biashara ya kimataifa maarufu
kama “Sabasaba”. (Picha na Zainul Mzige wa modewjiblog).
Mtaalam
wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce
Temu akimwelekeza mmoja wa wananchi aliyetembelea la Umoja huo jinsi ya
kuwasilisha maoni yake kuhusiana na kazi za Umoja wa Mataifa na nini
angependa Umoja huo ufanye zaidi kwa ajili ya watanzania.
Laurean
Kiiza (kushoto) kutoka kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC),
akimsimia Meneja mwendeshaji wa mtandao wa habari wa Modewjiblog,
Zainul Mzige kuwasilisha maoni (GeoPoll) yake moja kwa moja kwenye simu
ya kiganjani, alipotembelea banda la Umoja wa Mataifa kwenye maonyesho
ya sabasaba yanayoendelea kutimua vumbi jijini Dar es Salaam.
Mdau
wa mtandao wa habari wa Modewjiblog, Lemmy Hipolite (kulia) akipata
maelezo kutoka kwa Mkurugenzi na Meneja mradi wa TUBEGA ART ambaye ni
mtaalamu wa sanaa za uchoraji, Amos Mtambala, jinsi alivyowezeshwa na
Umoja huo kupitia Shirika la Kazi Duniani (ILO) kupata elimu
inayomwezesha kuwa mjasiriamali kwa kuuza michoro hiyo ndani ya banda la
Umoja wa Mataifa.
Mkurugenzi
na Meneja mradi wa TUBEGA ART ambaye ni mtaalamu wa sanaa za uchoraji,
Amos Mtambala, akionyesha baadhi ya kazi zake kwa wananchi waliotembelea
banda la Umoja wa Mataifa kwenye viwanja vya maonyesho ya 39 ya
biashara ya kimataifa maarufu kama “Sabasaba”.
Mtaalam
wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce
Temu akitoa maelezo ya maeneo mbalimbali yaliyofanikiwa katika
utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya Umoja wa Mataifa (UNDAP) kwa mmoja
wa wananchi aliyetembelea banda la Umoja wa Mataifa na kutaka kufahamu
shughuli mbalimbali za UN Tanzania.
Mtaalam
wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce
Temu akimkabidhi makabrasha na vipeperushi mbalimbali vya Umoja Mataifa,
Mwandishi wa Michuzi blog,
Chalila Kibuda aliyetembelea banda hilo kwenye maonyesha ya sabasaba
yanayoendelea katika viwanja vya Mwl. J.K Nyerere, barabara ya Kilwa,
jijini Dar.
Sophia
Mataro (wapili kushoto) kutoka Shirika la UNESCO Tanzania, akitoa
maelezo ya shughuli mbalimbali za Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini
kwa mmoja wa wananchi alitembelea banda la Umoja wa Mataifa lililopo
Karume Hall ndani ya viwanja vya maonyesho ya 39 ya biashara ya
kimataifa maarufu kama “Sabasaba”.
Afisa
Habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma
Ledama akizungumza na kituo cha Televisheni cha Channel Ten
kilichotembelea banda la Umoja wa Mataifa kwenye maonyesho ya Sabasaba
yanaoendelea kutimua vumbi jijini Dar es Salaam.
Timu
ya wafanyakazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa "Delivering as One"
wanaotoa huduma kwenye banda la Umoja wa Mataifa lililopo Karume Hall
kwenye viwanja vya maonyesho ya 39 ya biashara kimataifa maarufu kama
“Sabasaba” yanayoendelea kurindima jijini Dar es Salaam.
Muonekano
wa nje wa banda la Umoja wa Mataifa lililopo Karume Hall katika viwanja
vya Mwl. J.K Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.
Na Modewji blog team
Shirika
la Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania limetoa nafasi ya kipekee kwa
watanzania kutoa maoni yao wakati wa kipindi hiki cha maonyesho ya 39 ya
Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam, yaliyoanza kurindima Juni 28,
huku wakikusanya maoni mbalimbali kutoka kwa wananchi juu ya utendaji
wake kwa wanaotembelea kwenye maonyesho hayo kila siku.
Aidha,
katika kupokea maoni hayo, UN imeweka utaratibu wa moja kwa moja kwa
wananchi kufika kwenye banda lao na kutoa maoni yao, ambayo yanaenda
moja kwa moja kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) Nchini Alvaro Rodriguez.
Njia nyingine ya kuwasilisha maoni ya moja kwa moja ni kupitia mtandao wa (Online) kwa kuingia http://gpl.cc/UN2
Kupitia linki hiyo, mtumiaji anaweza kutumia simu yake ya smartphone, laptop na vifaa vingine vya kielektroniki.
Njia nyingine ni ya kutumia ujumbe mfupi wa maandishi (SMS), ambapo kwa watumiaji wa mtandao wa Airtel watatuma ujumbe wao kwenda namba 15453, kwa watumiaji wa mtandao wa Tigo wanatuma kwenda 15055 au 15453 na kwa Vodacom ni namba 15055.
Na kwa njia ya tatu ni kuwasilisha namba ya simu na majina na ujumbe unaotaka na UN wataufanyia kazi.
Aidha,
maoni hayo yatakuwa yakipokelewa kwa kipindi chote cha SabaSaba, hivyo
wananachi wameombwa kujitokeza kwa wingi kutoa maoni yao ya nini UN
wakifanye nchini pamoja na mambo mengine.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269