Mkurugenzi
wa masoko wa kampuni ya MeTL Group, Bi. Fatema Dewji-Jaffer akipokea
taarifa ya shughuli mbalimbali zinazoendelea kwenye maonyesho ya 39 ya
biashara ya kimataifa maarufu kama “Sabasaba” kwa mmoja wa maafisa wa
kampuni ya bidhaa za LG Tanzania ambapo kampuni ya Mohammed Enterprises
Limited Tanzania (MeTL) ndio msambazaji rasmi wa bidhaa hiyo nchini
kabla ya hafla fupi ya uzinduzi wa friji mpya ya LG yenye milango pacha
aina ya “Velvet Gardenia na Coral Irish”.
Mmoja wa wakurugenzi wa LG toka Korea, Bw. Billy Kim (Kulia) akizindua
rasmi friji mpya ya LG yenye milango pacha aina ya “Velvet Gardenia na
Coral Irish” katika banda la LG ndani ya viwanja vya maonyesho ya 39 ya
biashara ya kimataifa maarufu kama “Sabasaba” anayeshuhudia (kushoto) ni
Mkurugenzi wa masoko wa kampuni ya MeTL Group ambao ni mawakala pekee
wa usambazaji wa bidhaa za kampuni ya LG, Fatema Dewji-Jaffer.
Mkufunzi
mwandamizi toka kampuni ya LG Tanzania, Bi. Elizabeth Morris (katikati)
akifafanua zaidi kwa waandishi wa habari hawapo pichani aina mpya ya
friji ya LG yenye milango pacha aina ya “Velvet Gardenia na Coral Irish”
wakati wa uzinduzi wa bidhaa hiyo mpya, katika viwanja vya maonyesho ya
biashara ya kimataifa maarufu kama “Sabasaba”. Kulia ni Mkurugenzi wa
LG, Mohan Kumar na mmoja wa wakurugenzi wakuu wa LG toka Korea Bw. Billy
Kim pamoja na Mkurugenzi wa masoko wa kampuni ya MeTL Group ambao ni
mawakala pekee wa usambazaji wa bidhaa za kampuni ya LG, Fatema
Dewji-Jaffer (wa pili kushoto).
Na Modewjiblog team
Kampuni
ya LG Tanzania imetangaza ofa kabambe ya punguzo la bei za bidhaa zake,
itakayodumu katika kipindi chote cha maonyesho ya Kimataifa ya Biashara
ya Sabasaba ikiwa ni kuadhimisha mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Meneja
mwandamizi wa LG, Bw. Kim Taehoon amesema wateja watakaonunua bidhaa za
LG katika kipindi hiki cha Ramadhani na Sabasaba watafurahia punguzo la
bei la hadi asilimia 15, pamoja na ofa nyingine za kuvutia zikiwemo
zawadi za bure.
Bw.
Kim pia ametumia fursa hiyo kuitambulisha friji mpya za LG yenye
milango pacha aina ya “Velvet Gardenia” na “Coral Irish” kwa mara ya
kwanza kabisa katika soko la Tanzania na kuthibitisha kuwa kampuni ya
Mohammed Enterprises Limited Tanzania (MeTL) kuwa msambazaji rasmi wa
bidhaa hiyo nchini.
Amesema
friji hizo zina nafasi kubwa na nyingi za kuhifadhia vyakula, uwezo wa
kuzuia bakteria na hivyo kutunza vyakula katika hali ya usalama wa
kiafya.
Friji hizo zina makabati yaliyojengewa kwa ndani katika milango yake, ambapo aina hiyo ya milango huja pamoja na kioo imara.
Amesema
friji hizo zinatumia teknolojia mpya ya LG “Smart Inverter Compressor”
ambayo ina uwezo wa kupunguza matumizi ya umeme hadi asilimia 36.
Bw.
Kim amewashauri watanzania kuchangamkia fursa ya bidhaa hizo mpya
zilizoingia sokoni na kuwahakikishia kuwa watastaajabishwa na ubora na
uwezo wa friji hizo,
Amesema kuwa Friji hizo pia zitapatikana katika maduka mengine yote yanayouza vifaa vya kielektroniki jijini Dar es Salaam.
Ameongeza
kuwa katika kipindi hiki cha mfungo mtukufu wa Ramadhani, watu wengi
hutunza vyakula vyao kwenye friji na ni hulka ya wengi kuamka usiku kwa
ajili ya kupata Daku, hivyo bidhaa hii itakuwa na manufaa sana kwao,
kwani ina uwezo wakulinda dhidi ya unyevunyevu na pia kutunza chakula
katika hali ya usalama.
Ofa
hizi zitadumu kipindi chote za mwezi mtukufu wa ramadhani pamoja na
Sabasaba, hii ni katika kuwapa wateja wa LG muda wa kutosha kujipatia
bidhaa za LG zenye punguzo la bei
Bw.
Kim Taehoon amesisitiza kuwa kampuni ya LG Electronics daima inaendelea
kuboresha mfumo wa teknolojia ili kuleta bidhaa zenye ubora na
muonekano yakinifu, ili kufikia viwango vya matumizi ya kimataifa.
Amesema
toka kuanzishwa kwake mwaka 1958, LG inaendelea kuzalisha bidhaa
zinazoendana na mahitaji ya wateja wake na uingizwaji wa bidhaa hii mpya
sokoni ni muendelezo wa matoleo ya teknolojia, ambayo yanatengenezwa na
kuboreshwa kulingana na matakwa na mahitaji ya wateja.
Mkufunzi
mwandamizi toka kampuni ya LG, Elizabeth Morris, (kushoto) akiwaonyesha
waandishi wa habari (hawapo pichani) ubora wa kompresa za friji za
kampuni ya LG ambazo ni imara na zinahimili hali ya hewa ya mazingira
yoyote wakati wa uzinduzi wa bidhaa hiyo mpya katika viwanja vya
maonyesho vya sabasaba.
Mkufunzi
mwandamizi toka kampuni ya LG, Elizabeth Morris, (kushoto) akiwaonyesha
waandishi wa habari (hawapo pichani) bidhaa nyingine za LG ambazo zipo
kwenye ofa ya punguzo la bei la asilimia 15 katika msimu huu wa sabasaba
na Ramadhani ndani ya banda la MeTL Group.
Waandishi
wa habari wakiangali moja ubora wa TV za LG kwa kutumia miwani ya 3D
inapoivaa inakuonyesha uhalisia wa picha unayoitaza kwa ukaribu zaidi
wakati uzinduzi wa moja ya bidhaa za LG katika banda la kampuni ya MeTL
Group kwenye maonyesho ya sabasaba yanayoendelea kutimua vumbi jijini
Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa masoko wa kampuni ya MeTL Group ambao ni mawakala pekee wa
usambazaji wa bidhaa za kampuni ya LG, Fatema Dewji-Jaffer akimkabidhi
zawadi kutoka MeTL, Mkurugenzi wa kampuni ya LG toka Korea, Bw. Billy
Kim mara baada ya uzinduzi huo katika banda la MeTL Group.
Mkurugenzi
wa masoko wa kampuni ya MeTL Group ambao ni mawakala pekee wa
usambazaji wa bidhaa za kampuni ya LG, Fatema Dewji-Jaffer akiendelea na
zoezi la kukabidhi zawadi kwa maafisa wa kampuni ya LG Tanzania.
Meneja
wa LG tawi la Nkurumah, Bw. Yasin Lodhi akizungumza na waandishi wa
habari ambapo ametumia fursa hiyo kuwakaribisha watanzania kutembelea
banda la LG na kununua bidhaa mbalimbali zenye ubora wa hali juu na zipo
katika punguzo la bei la asilimia 15 ya kila bidhaa katika kipindi
hichi cha sabasaba na mwezi huu wa Ramadhani.
Mkufunzi
mwandamizi toka kampuni ya LG, Elizabeth Morris akizungumza na
waandishi wa habari mara baada ya uzinduzi huo. Wa tatu kulia ni Meneja
wa LG tawi la Nkurumah, Bw. Yasin Lodhi.
Mkurugenzi
wa masoko wa kampuni ya MeTL Group, Fatema Dewji-Jaffer katika picha ya
pamoja na wafanyakazi wa kampuni ya LG Tanzania na MeTL Group wanaotoa
huduma kwenye cha maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba
yanayoendelea kutimua vumbi viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara
ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269