Mwenyekiti wa Makampuni ya Hoteli ya Mark and High Class
Group Tanzania Rustam Merani akizungumza na Wageni na Wadau mbalimbali
(hawapo pichani) mara baada ya kuzinduliwa Hoteli ijulikanayo kama
‘TAUSI Palace’ iliyopo Shangani, Mji Mkongwe Zanzibar.
Picha zote na Makame Mshenga.
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Utalii na Michezo Saidi Ali Mbarouk akizungumza na Wadau mbalimbali mara
baada ya kuzinduliwa Hoteli ijulikanayo kama ‘TAUSI Palace’ iliyopo
Shangani, Mji Mkongwe Zanzibar. Picha zote na Makame Mshenga.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Saidi Ali Mbarouk akikata utepe
kuashiria ufunguzi wa Hoteli Mpya “Tausi Palace” iliyokua Chavda Hoteli
iliyopo Shangani Mjini Zanzibar (kushoto) Mwenyekiti wa Makampuni ya Hoteli ya Mark and High Class Group Tanzania Rustam Merani.
Mwenyekiti wa Makampuni ya Hoteli ya Mark and High Class Group Tanzania
Rustam Merani akimuonesha moja ya vyumba cha Hoteli hiyo Waziri wa
Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Saidi Ali Mbarouk mara baada ya
kuizundua rasmi.
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Utalii na Michezo Saidi Ali Mbarouk (kulia) akiwa na mwenyeji wake
Mwenyekiti wa Makampuni ya Hoteli ya Mark and High Class Group Tanzania
Rustam Merani wakingia katika Hoteli yao mpya ya Tausi Palace iliyopo Shangani Mjini Zanzibar.
…………………………………………………………………………
Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar
Upatikanaji wa huduma bora za
Kiutalii ikiwemo Hoteli za kisasa ni miongoni mwa Vivutio muhimu vya
Watalii kuja kuitembelea Zanzibar.
Hayo yameelezwa na Waziri wa
Habari,Utamaduni,Utalii na Michezo Zanzibar ,Said Ali Mbarouk katika
uzinduzi wa Hoteli ijulikanayo kama TAUSI Palace iliyopo Mji Mkongwe
mjini, Zanzibar.
Amesema Utalii imara huambatana
na huduma bora na kwamba uwepo wa Tausi Palace utasaidia ongezeko la
Watalii na kupelekea kuimarika zaidi Sekta hiyo.
Waziri Mbarouk amesema kwa sasa
Sekta hiyo inaajiri zaidi ya watu Elfu 20, na kuchangia kwa kiasi
kikubwa ongezeko la Pato la taifa.
Amefahamisha kuwa Serikali
itaendelea na juhudi zake za kuwahamasisha Wawekezaji kuwekeza katika
Sekta hiyo ili kuzidi kuimarisha Uchumi wa Zanzibar.
Amesema Zanzibar ina vivutio
Vingi vya Utalii na mazingira salama ya kiuwekezaji na kuwaomba
Wawekezaji hao kuendelea kutumia fursa hiyo ili iweze kuwanufaisha wao
na Jamii kwa ujumla.
Waziri Mbarouk amesema anaamini
Ubora wa Hoteli hiyo utapelekea Watalii mbalimbali wanaofika Zanzibar
kufika katika Hoteli hiyo na kujionea Ubora wa huduma zake.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
Kampuni ya Hoteli za “Mark and High Class Group” inayomiliki Hoteli
mbalimbali Zanzibar na Tanzania Bara amesema lengo lao ni kutoa huduma
bora za kiutalii ili ziwanufaishe na kuisaidia jamii ya Zanzibar.
Amesema Kampuni yao imevutika na
Vivutio vingi vya kiutalii Zanzibar sambamba na hali ya utulivu na amani
iliyopo jambo ambalo litapelekea Sekta hiyo kupiga hatua siku hadi
siku.
Aidha amesema wapo njiani kujenga Hoteli bora ya Nyota tano katika Eneo la Mbweni ifikapo June mwakani.
Kwa upande wake Meneja Mkuu wa
Hoteli hiyo John Kiruthi amesema ubora wa huduma zao na kujitangaza
vyema katika Soko la Utalii la Dunia ndiko kutakakopelekea kupata wageni
wengi katika Hoteli hiyo.
Aidha amesisitiza kuwa
watahakikisha agizo la kuajiri Asilimia 30 ya Wafanyakazi kutoka
Zanzibar linatekelezwa ili kuisaidia Serikali kupunguza tatizo la Ajira
kwa Vijana.
Miongoni mwa mambo ya upekee ya
Hoteli hiyo ni pamoja na kuwepo kwa Vyumba Vikubwa, Ukumbi mkubwa wa
Mikutano na Wahudumu wakarimu.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269