Subject: TBL YAKABIDHI MSAADA WA KISIMA CHA SH. MIL. 65 RUFIJI
To: Ahmad Michuzi , fadhili athumani , "info@dewjiblog.com" , Othman Michuzi , Cathbert Kajuna , King Jofa , Andrew Kevin Mbega , Haki Ngowi , Luke Joe , Subi Nukta , Josephat Lukaza , Jamvi la Habari Tanzania , Francis Dande , mzige , Blog za mikoani , zainul@modewjiblog.com, "uwazi@hotmail.com" , Daniel Mbega , Bashir Nkoromo , Bukoba Wadau , Bongoclan Tanzania Tv , Jestina George , Adam Mzee , verbs@rocketmail.com, Deogratius Rweyunga , Aloyson Jr , Gadiola Emanuel , Richard Mwaikenda
Mkuu
wa Wilaya ya Rufiji , Nurdin Babu akiwa na Mkurugenzi wa Sheria na
Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), wakifungua maji ya bomba mara
baada ya makabidhiano ya kisima kilichochimbwa na TBL kwa gahrama ya
shilingi mil. 65 katika Kijiji cha Mwaseni Wilaya ya Rufiji, mkoani
Pwani. Makabidhiano hayo yalifanyika kijijini hapo mwishoni mwa wiki.
Mkuu
wa Wilaya ya Rufiji, Nurdin Babu akiwa na Mkurugenzi wa Sheria na
Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Stephen Kilindo, wakiwatwisha
ndoo za maji akina mama wa Kijiji cha Mwaseni, Mibuyu Saba mara baada
ya kukabidhi kisima cha maji kilichochibwa na TBL kwa gharama ya
shilingi mil. 65, wilayani RufijiMkoa wa Pwani. Hafla hiyo ilifanyika
kijijini hapo mwishoni mwa wiki.
Mkuu
wa Wilaya ya Rufiji, Nurdin Babu akiwa na Mkurugenzi wa Sheria na
Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Stephen Kilindo, wakiwatwisha
ndoo za maji akina mama wa Kijiji cha Mwaseni, Mibuyu Saba mara baada
ya kukabidhi kisima cha maji kilichochibwa na TBL kwa gharama ya
shilingi mil. 65, wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani. Hafla hiyo ilifanyika
kijijini hapo mwishoni mwa wiki.
Na Mwandishi wetu , Rufiji
MKUU
wa wilaya ya Rufiji, Nurdin Babu amewataka wakazi wa kijiji cha
mwaseni Mibuyu saba kulinda miradi mbalimbali ya maendeleo hili kuweza
kupunguza tatizo la umaskini katika eneo hilo.
Babu
alisema hayo alipokuwa akizungumza na wakazi wa kijiji hicho wakati wa
makabidhiano ya Kisima kirefu cha maji safi kilicho chimbwa na Kampuni
ya bia Tanzania (TBL) kwa ajili ya wakazi eneo hilo
“Kisima
hiki ni sehemu ya miradi ya maendeleo ambayo imekuwa ikifadhiliwa na
TBL katika jamii hivyo sio kitu cha itikadi kila mtu anapaswa kukitunza
na kulinda kwa ajili ya kupunguza mzigo wa
kwenda kufata maji mbali kwa wakina mama waishio hapa” alisema Babu.
Babu
aliongeza kuwa mbali ya kuchota maji tu lazima kijiji kiweke utaratibu
wa kuakikisha kuwa kila mmoja anachangia huduma kidogo hili kuweza
kufanya huduma hiyo kuwa endelevu na sio ikiaribika kusubiri kutafuta
mfadhili tena.
Akziungumza
wakati wa kukabidhi kisima hicho Mkurugenzi wa Sheria na Mahusiano
kutoka TBL, Stephen Kilindo alisema kuwa mradi huo umegharimu kiasi cha
fedha shilingi milioni 65 za kitanzania na kukabidhiwa kwa wana kijiji
hao.
Alisema
kuwa kisima hicho kirefu ambacho kimesambaza mabomba manne ya kutolea
maji kitaweza kuhudumia watu 1700 waishio katika eneo hilo na maeneo ya
jirani.
Kilindo
alisema TBL kama mdau wa maendeleo na shirika ambalo uwepo wake
inategemea watanzania imeamua kuchimba kisima hicho kama ni sehemu ya
kurudisha kile wanacho kipata kwa wananchi hili waweze kufurahia miasha
kama ilivyo katika nchi zingine duniani.
“Tanzania
kilamahala kuna maji kinachohitajika ni uwezeshaji hivyo sisi kama TBL
tumeliona hilo ndio maana tumeamua kujenga visima kila mahali palipo
kuwa na mahitaji ya maji hapa nchini” alisema Kilindo.
Kwa
upande wake mwenyekiti wa kijiji cha Mwaseni Mibuyu Saba, Hasan
Abdallah alishukuru TBL kwa msaada huo mkubwa katika kijiji chake kwa
kusema kuwa wameweza kutatu changamoto kubwa katika eneo ambayo inaweza
kuwa chachu ya maendeleo mingine yote.\
Alisema
kuna mashirika mengi sna lakini TBL kwa moyo wao wameweza kuona tatizo
la mwaseni na kulibeba kama lao hivyo awana neon zaidi ya shukrani
katika kampuni hiyo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269