Muandaaji
wa Filamu ya Wake-Up, Manaiki Sanga (katikati), akizungumza katika
mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu filamu
hiyo mpya inayotarajiwa kuzinduliwa Agosti 30, 2015. Kulia ni msanii wa
filamu, Farida Sabua 'Mama Sonia na Salim Ahmed 'Gabo'.
Msanii wa filamu, Taiya Odero (kulia), akizungumza
katika mkutano huo.
Meza kuu. Kutoka kulia ni Taiya Odero, Farida Sabua 'Mama Sonia, Muandaaji wa Filamu ya Wake-Up, Manaiki Sanga , Salim Ahmed 'Gabo na Kaushik Surelia.
Msanii wa filamu, Salim Ahmed 'Gabo' (kushoto), akizungumza katika mkutano huo.
Msanii Farida Sabua 'Mama Sonia (kulia), akichangia jambo kwenye mkutano huo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Na Dotto Mwaibale
WATANZANIA
na wadau wa filamu wameomba kuunga mkono filamu mpya ya Wake-up ambayo
inatarijiwa kuzinduliwa Agosti 31, 2015 jijini Dar es Salaam.
Mwito
huo umetolewa na muandaaji wa filamu hiyo Manaiki Sanga wakati
akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu
filamu hiyo.
"Filamu
hii ni ya aina tofauti na filamu ambazo zimefanywa hapa nchini kwani
imewashirikisha mastaa wa bongo movie 31 na imetengenezwa kwa ubora wa
hali ya juu" alisema Sanga.
Alisema
maudhui ya filamu hiyo yamehusu zaidi familia na inaweza kuonwa na watu
wa rika lote na imezingatia maadili na utamaduni wa kitanzania.
Sanga
aliwataja baadhi ya wasanii waliocheza filamu hiyo kuwa ni Mzee Majuto,
Irene Uyowa, Hemed PHD, Quick Rock, Frola Mvungi, Asha Boke, Mama
Sonia, Gabo, Prince Kas na wengine wengi.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269