Mgombea
nafasi ya kuwania ubunge Jimbo la Kawe, Wakili Elias Nawera (kushoto),
akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo
asubuhi.
Mgombea
nafasi ya kuwania ubunge Jimbo la Kawe, Wakili Elias Nawera (kushoto),
akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo
asubuhi, kuhusu kumpa ushirikiano mgombea wa nafasi hiyo aliyeshinda
kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika jimbo hilo na
kukamatwa kwake na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru)
kwa madai ya kutoa rushwa.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Na Dotto Mwaibale
MGOMBEA
nafasi ya kuwania ubunge Jimbo la Kawe, Wakili Elias Nawera amesema
atampa ushirikiano mgombea wa nafasi hiyo aliyeshinda kura za maoni
ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuhakikisha CCM inapata ushindi.
Nawera
aliyasema hayo jijini Dar es Salaam leo asubuhi wakati akizungumza na
waandishi wa habari kuhusu mchakato wa kura za maoni katika jimbo hilo
na kuhusishwa na kukamatwa kwake na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa (Takukuru) kwa madai ya kutoa rushwa.
"Nampongeza
mwenzangu aliyeongoza kura za maoni katika jimbo la Kawe na ninaahidi
kushirikiana na mgombea mwenzangu atakaye teuliwa na vikao vya uteuzi
vya CCM kupeperusha bendera katika uchaguzi mkuu na kuwa ushindi wa
kishindo kwa CCM kuanzia udiwani, ubunge na urais". alisema Nawera.
Akizungumzia
kuhusu mchakato huo na kuhusishwa na rushwa aliilalamikia Takukuru kwa
kumuhusisha na tukio hilo kuwa walikuwa na nia ya kumsaidia mmoja wa
wagombea nafasi hiyo na yeye kumpunguza nguvu kisiasa.
Nawera
alisema licha ya kutoa taarifa za vitendo vya rushwa katika mchakato
huo hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa lakini katika mazingira ambayo
hakuyategemea amebambikiwa tuhuma hizo ambazo hakuwa nazo.
Aliongeza
kuwa wakati wa ukamatwaji wake hawakumjulisha kuwa yupo chini ya
ulinzi, pia hawakujitambulisha na wala hawakumuambia anatuhumiwa kwa
kosa gani na bila kumpa nafasi ya kuwasiliana na ndugu zake au
mwanasheria na kumpeleka kituo cha polisi Magomeni.
Nawera
alisema si jambo zuri kwa vyombo vya dola kumkamata mwananchi na
kumuhusisha na tuhuma mbalimbali hiyo si sahihi na ni matumizi yasiyofaa
ya rasilimali za nchi na matumizi mabaya ya madaraka.
Muwania
ubunge huyo Julai 30, 2015 saa mbili usiku alikamatwa na maofisa wa
Takukuru kwa kuhusishwa na rushwa na baada ya mahojiano alisweka rumande
kwa masaa 10 na kuachiwa kwa kujidhamini mwenyewe.
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269