Breaking News

Your Ad Spot

Aug 19, 2015

RAIS WA GABON AMETOWA URITHI WAKE KWA UMMA


Rais wa Gabon ametoa urithi wake kwa vijana wa Gabon
Rais wa Gabon Ali Bongo Ondimba ameahidi kutoa urithi wake wote kwa vijana nchini humo.
Ali anasema kuwa mali yote aliyopokea kama urithi kutoka kwa babake mzazi aliyekuwa rais wa Gabon kwa kipindi kirefu,Omar Bongo itakwenda kwa vijana wa Gabon.
Shirika la habari la AFP limesema kuwa rais Bongo ameahidi kuuza mijengo miwili iliyoko Ufaransa aliyopewa na babake kwa thamani ya Franka moja kama ishara ya kujitolea kuimarisha hali ya kiuchumi ya vijana wa taifa.
Jumba moja la kifahari lililoko katika mji mkuu wa taifa hilo litabadilishwa na kuwa chuo kikuu cha Umma.
Majumba mengine mawili yako mjini Paris Ufaransa.BBC

Majumba mawili yako mjini Paris Ufaransa na lingine liko Gabon.
Kauli hiyo ya rais Bongo inawadia wakati ambao majaji nchini Ufaransa wamekuwa wakifuatilia na kuchunguza chanzo cha mamilioni ya fedha zilizotumika kununua na kujenga majumba ya kifahari nchini humo.
Wapinzani na wanaharakati wa kupambana na ufisadi wanasema kuwa huenda rais Ali Bongo Ondimba ameona kibano kinachokuja akaamua kuirejeshea taifa mali yake.
Shirika la kupigana na ufisadi, Transparency International liliwasilisha kesi mahakamani likitaka majaji hao waamuru kuwa mali ya umma ilitumika kujistawisha wakati wa utawala wa babake marehemu rais Omar Bongo.
Babake marehemu rais Omar Bongo alitawala nchi hiyo kwa miaka 40.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages