Breaking News

Your Ad Spot

Sep 24, 2015

AMATWA NA VIUNGO VYA BINADAMU, NYARA ZA SERIKALI SINGIDA

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida, ACP Thobias Sedoyeka.Vipande viwili vya fuvu la binadamu.Chupa tatu za mafuta ya simba alizokutwa nazo mtuhumiwa.
Vipande vya ngozi ya simba
JESHI la polisi mkoani Singida linamshikilia mkazi moja wa Kijiji cha Itumba, wilaya ya Igunga, mkoani Tabora kwa tuhuma za kukutwa na viungo vya binadamu na nyara za serikali.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida, ACP Thobias Sedoyeka, amemtaja mtuhumiwa kuwa ni Magida Bundala aliyekamatwa akitoka mkoani Tabora kuja Singida kusalimia ndugu zake ambao walikuwa wamewekwa mahabusu katika Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Ikungi.
Kamanda Sedoyeka alisema walimkamata mtuhumiwa huyo baada ya askari kumtilia mashaka na kuamua kumkagua wakati akisubiri kuwasalimia ndugu zake ambao ni mahabusu alipokutwa na vipande viwili vya fuvu la binadamu, ngozi ya chatu, vipande vya ngozi ya simba, pembe ambayo haijajulikana kuwa ni ya mnyama gani na chupa tatu za mafuta ya simba.
Wakazi wa Manispaa ya Singida wameliomba jeshi la polisi kuhakikisha linamfuatilia mtuhumiwa huyo ili kubaini mtandao mzima kwa sababu unaendesha shughuli zao kutokana imani potofu ikiwa ni pamoja kupata madaraka, jambo ambalo husababisha vifo kwa binadamu wakiwemo walemavu wa ngozi (albino).
CHANZO: ITv

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages