Breaking News

Your Ad Spot

Sep 24, 2015

MAGUFULI APIGWA NA BUTWAA UMATI WA WATU GEITA, AAHIDI KUSHUGHULIKIA MATATIZO YA WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania   kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi katika mkutano wake wa kampeni  uliofanyika katika uwanja wa shule ya Msingi Kalangalala mjini Geita leo na kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi.

Mgombea Urais huyo amewaambia wananchi wa Geita kuwa mara atakapoingia Ikulu, moja ya changamoto anazotarajiwa kuzipa kipaumbele ni pamoja na suala la kutatua mgogoro wa wachimbaji madini wadogo wadogo.

Magufuli ameasema kuwa akiingia madarakani atawapa maeneo wachimbaji wadogo wa madini nchini ikiwa ni pamoja na kuwakopesha mitaji na kuwapa vifaa vya kisasa vya kufanyia kazi zao pamoja na mafunzo kwa ajili ya  kuboresha uchimabaji wao ili uwe wa kisasa zaidi na kupandisha  kiwango cha  ufanisi wa kazi zao za uchimbaji.

Dkt. Magufuli jana alihutubia mikutano katika miji ya Runzewe wilayani Bukombe, Katoro wilayani Chato na Geita mjini akiendelea na kampeni zake za kwaomba wananchi kumpa kura za ndiyo ili aweze kuingia Ikulu na kuwafanyia kazi Watanzania kama kiongozi na Amiri Jeshi mkuu wa Tanzania. 
Sehemu ya umati wa wakazi wa Geita na vitongoji vyake wakiwe kwenye mkutano wa kampeni wa Dkt John Pombe Magufuli uliofanyika jioni ya jana mjini humo. (Picha zote na Michuzi JR-Geita)
Wananchi wa mji wa Geita na vitongoji vyake wakiwa wamefurika kwenye uwanja wa shule ya msingi ya Kalangalala, wakimsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia chama cha Mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akijinadi na kumwaga sera zake mbele za wananchi hao ikiwemo pia na kuwaomba ridhaa ya kuwa Rais kwa kushinda kura nyingi ifikapo Oktoba 25 mwaka huu,ambapo uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika

Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwandani Wagombea Ubunge wa jimbo la Busanda Mh. Lolensia Bukwimba na Dkt Meedad wa Chato mapema mchana huu alipokuwa akiwahutubia wananchi wa mji mdogo wa Katoro mkoani Geita, kwenye viwanja vya mnada wa Ng'ombe, katika mkutano wa hadhara wa kampeni, ambapo maelfu ya Wananchi wamehudhuria. Dkt Magufuli atahutubia jioni ya leo mjini Geita kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa mji mdogo wa Katoro mkoani Geita mapema leo mchana kwenye viwanja vya mnada wa Ng'ombe, kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni, ambapo maelfu ya Wananchi wamehudhuria.
Wananchi wa Runzewe wilaya ya Mbongwe mkoani Geita wakimsikiliza kwa makini Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akizinadi sera zake na kuwaomba ridhaa ya kuiongoza Tanzania katika kipindi cha awamu ya tano, kwenye viwanja vya mnada wa Ng'ombe, katika mkutano wa hadhara wa kampeni, ambapo maelfu ya Wananchi wamehudhuria. 
Wananchi wa Runzewe wakimsikiliza Dkt Magufuli alipokuwa akihutubia kwenye mkutano wa kampeni.
Wananchi wa Runzewe wakimshangilia Dkt Magufuli alipokuwa akijinadi na kuomba kurra za ushindi ili aweze kuwa Rais wa Tanzania katika awamu ya tano.
Wakiwa na mabango yao wakishangilia ujio wa Magufuli.
Wananchi wa Runzewe wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipokuwa akijinadi na kuomba kurra za ushindi ili aweze kuwa Rais wa Tanzania katika awamu ya tano.
Magufuli Style ilitikisa pia ndani ya Geita kwenye mkutano wa kampeni wa Dkt John Pombe Magufuli jioni ya jana.????????????????????????????????????
Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. John Pombe Magufuli akikumbatiana kwa furaha na kijana mlemavu wa ngozi Albino Lazaro Malendeka ambaye alikuwa mtumishi wa kikundi cha Red Briged cha Chadema baada ya kujiunga na CCM mjini Geita jana.
????????????????????????????????????
Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania   kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwapokea  mlemavu wa ngozi Albino Lazaro Malendeka kushoto ambaye alikuwa mtumishi wa kikundi cha Red Briged cha Chadema baada ya kujiunga na CCM mjini Geita jana na William Mabula Msalaba aliyekuwa mgombea ubunge wa Chadema jimbo la Geita.
????????????????????????????????????
Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania   kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwanadi wagembea ubunge wa mkoa wa Geita katika mkutano wa kampeni uliofanyika mjini Geita jana.
Wananchi wa Katoro wakiushangilia msafara wa Dkt Magufuli alipokuwa akielekea kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
Msafara wa Mgombea Urais ukielekea kwenye mkutano wa hadhara ndani ya mji Mdogo wa Katoro mkoani Geita. 
Umati wa watu.
Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania   kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Geita Mama Fatma Mwasa. Pichani katikati ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza na Mjumbe wa kamati ya ushindi ya CCM mjini Geita wakati wa mkutano wa kampeni leo
Wakazi wa Geita wakishangilia jambo kwenye mkutano huo wa kampeni.

Wananchi wa Geita mjini wakifuatilia mkutano wa kampeni.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita na mgombea ubunge wa jimbo la Geita vijijini Ndugu Joseph Kasheku a.k.a King Msukuma akihutubia malefu ya wananchi wa Geita mjini kwenye mkutano wa kampeni wa Urais, ambapo Ndugu Joseph aliwaomba wakazi wa Geita na vitongoji vyake kumchagua Dkt John Pombe Magufuli awe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika awamu ya tano,katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 25 mwaka.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Shinyanga mjini Ndugu Steven Masele akimwombea kura Mgombea Urais wa CCM Dkt. Magufuli kwa wakazi wa Geita
Umati wa watu ukishangilia.
Wananchi wa Geita mjini wakimsikiliza Dkt Magufuli alipokuwa akiwahutubia jioni ya jana kwenye mkutano wa kampeni.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi wa Nyakahura, Wilaya ya Biharamulo alipokuwa akielekea mkoani Gieta kuendelea na kampeni zake.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages