Imekuwa ni sadfa ya aina yake baada
ya dada watatu kujifungua siku moja nchini Ireland, wa nne naye
akitarajia kujaliwa mtoto wakati wowote.
Watoto hao watatu wote walizaliwa hospitali ya Mayo mjini Castlebar katika Kaunti ya Mayo Jumanne.
Dada
hao ambao hukaa karibu sana eneo la Cloonfad, kaunti ya Roscommon,
walisema hawakuwa wamepanga kujaliwa watoto wakati mmoja.
Wahudumu katika hospitali hiyo walisema watoto wote watatu wako buheri wa afya.
Mairead FitzPatrick alikuwa wa kwanza kujifungua, akimpata mvulana kwa jina Thomas Óg, saa 03:25 saa za huko.
Dadake
Joeline Godfrey alijifungua msichana kwa jina Sorcha mwendo wa saa
11:00, naye wa tatu, Bernie Ward, akajifungua mvulana aliyepewa jina
Phelim saa 20:30.
Dada yao mwingine, Christina Murray, pia amelazwa hospitali hiyo akitarajiwa kujifungua wakati wowote.
Dada asikitika
Bi Murray alisema amesikitika "kiasi" kwamba hakujifungua siku moja na wenzake, lakini anatumai atampata mtoto wake karibuni.
Bi
FitzPatrick aliambia kituo cha habari cha RTÉ nchini Ireland, kuwa
ingawa wote walitarajiwa kujifungua muda unaokaribiana, hawakudhani
wangejaliwa watoto katika kipindi cha saa 24.
"Siku yangu ya kujifungua ilifaa iwe Ijumaa, 28 Agosti, na Christina alifaa kujifungua tarehe 30,'' akasema.
Aliongeza
kuwa Joeline alijifungua kwa kufanyiwa upasuaji siku ya Jumanne ili
hali Bernie, aliyefaa kujifungua siku ya Jumatano Septemba 2,
alijifungua siku moja mapema.
Meneja anayesimamia kitengo cha kina
mama kujifungua katika hospitali hiyo, Mary Salmon, alisema wahudumu
walishangazwa na sadfa hiyo.
"Sote twalizungumzia hilo hali kwamba
tuna dada wanne hapahospitalini na hili halijawahi kufanyika, kadiri ya
ufahamu wetu." Alisema Bi Salmon.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269