Huku uchina ikiadhimisha miaka
sabini tangu ilipoishinda Japan katika vita vya pili vya dunia, marais
wa Afrika Kusini na Sudan, ambao wanahudhuria sherehe hizo, wamefanya
mkutano wa ghafla kujadili uhusiano kati ya nchi hizo mbili.
Mara
ya mwisho wawili hao wakikutana, kiongozi wa Sudan Omar al Bashir,
alikuwa akihudhuria mkutano wa wakuu wa serikali wa Muungano wa Afrika
AU, mjini Johannesburg Juni mwaka huu.
Lakini kiongozi huyo
aliondokwa kwa ghafla baada ya shirika moja lisilo la kiserikali kwenda
mahakamani, kutaka kiongozi huyo wa Sudan akamatwe na kuwasilishwa kwa
mahakama ya kimataifa ya ICC.
Bashir anakabiliwa na mashtala ya mauaji ya halaiki na uhalifu wa kivita ambao ulisababisha vifo vya zaidi ya watu laki tatu.
Mkutano
huo sasa umeashiria kuwa kesi hiyo iliyowasilishwa mahakamani nchini
Afrika Kusini, ya kutaka kiongozi huyo wa Sudan akamatwa haijaadhiri
uhusiano kati rais Omar al Bashir na rais Jacob Zuma.
Taarifa
kutoka kwa ofisi ya rais Zuma imesema kuwa wawili hao walijadili masuala
kadhaa ikiwemo kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili.
Sudan
na Afrika Kusini zimesaini mikataba 16 ya ushirikiano katika secta ya
kilimo, nishati, miundo mbinu, sayansi na technolojia.
Rais Zuma pia amekubali mwaliko wa rais Bashir kuzuru Sudan
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269