Breaking News

Your Ad Spot

Sep 5, 2015

DK MAGUFULI KUWANYANG'ANYA ARDHI VIGOGO WALIOJILIMBIKIZIA, ATAIGAWA KWA WAKULIMA NA WAFUGAJI


 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akikimbia kuonesha ukakamavu kwenda jukwaani kujinadi wakati wa mkutano wa kampemi  katika Uwanja wa Taifa mjini Ifakara wilayani Kilombero, Mkoa wa Morogoro leo. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli akijinadi kwa wananchi katika mkutano wa kampeni uliofanyika Mjini Ifakara, wilayani Kilombero, Morogoro. Dk Magufuli jana alifanya pia kampeni katika wilaya za Ulanga na Malinyi.

Akihutubia kwa nyakati tofauti katika Wilaya za Ulanga, Malinyi na Kilombero, Dk Magufuli amesema kuwa akipta ushindi atawanyang'anya ardhi vigogo wote waliojilimbikizia ardhi bila kujiendeleza na kuigawa kwa wakulima na wafugaji nchini.
 Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli akijinadi akifanananisha upara wake na wa Mgombea Ubunge wa Jimbo jipya la Malinyi katika mkutano wa kampeni uliofanyika jana katika Kata ya Mtimbila Wilaya mpya ya Malinyi, Morogoro. Dk Magufuli  alifanya pia kampeni katika wilaya za Ulanga na Kilombero

 Mmoja wa wananchi akiwa na bango linalosema Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli anasubiri kuapishwa tu katika mkutano wa kampeni uliofanyika jana Mjini Ifakara, wilayani Kilombero, Morogoro. Dk Magufuli alifanya pia kampeni katika wilaya za Ulanga na Malinyi.

 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli akikagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Kilombero alipokuwa akitoka kufanya kampeni katika Wilaya za Ulanga na Malinyi kwenda   Mjini Ifakara, wilayani Kilombero, Morogoro.

 Mmoja wa wafuasi wa CCM akiwa na picha ya Dk Magufuli mjini Mahenge, wilayani Ulanga

 Wananchi wakishangilia baada ya kufurahishwa na hotuba ya Dk Magufuli mjini Mahenge, Ulanga

 Madini wakinadiwa na Dk Magufuli wakati wa mkutano wa kampeni mjini Mahenge leo

 Dk Magufuli akiombewa na mmoja wa masheikh baada ya kumaliza kujinadi kwa wananchi mjini Mahenge Ulanga

 Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli akimpatia zawadi mtoto alipokuwa akiondoka mjini Mahenge wilayani Ulanga, baada ya kufanya mkutano wa kampeni

 Wananchi waliouzuia msafara wa Dk Magufuli katika Kijiji cha Ilagua Mission, Wilaya mpya ya Malinyi ukielekea Kata ya Mtimbila.

 Moja ya mabango yaliyishikwa na wananchi katika mkutano wa kampeni katika Kata ya Mtimbila, wilayani Malinyi leo

 Wananchi wakishangilia wakati Dk Magufuli akiwasili kwenye mkutano wa kampeni katika Kata ya Mtimbila

 Dk Magufuli akijinadi kwa wananchi katika Kata ya Mtimbila, wilayani Malinyi

 Mwananchi akitafakari wakati Dk Magufuli akihutubia na kutoa ahadi ikiwemo ya kuanzisha malipo ya pensheni kwa wazee nchini

 Hureee Dk Magufuli

 Dk Magufuli akimnadi Mgombea ubunge Jimbo la Malinyi, Dk. Harji Mponda wakati wa mkutano huo

 Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Ulanga, mkoani Morogoro, Said Kitila akitangaza kukihama chama hicho na kujiunga na CCM katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika Kata ya Mtimbila, wilaya mpya ya Malinyi, mkoani Mororogoro

 Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema wa Uratibu wa Msingi Wilaya ya Ulanga, Evance Tagala akionesha kadi kabla ya kuikabidhi kwa Dk Magufuli alipotangaza kukihama chama hicho na kujiunga na CCM wakati wa mkutano huo wa kampeni katika Kata ya Mtimbila.

 Tagala akipongezwa na wafuasi wa CCM baada ya kujiunga na chama hicho

 Wananchi wakimsikiliza Dk Magufuli alipokuwa akijinadi katika Kijiji cha Lupilo wilayani Ulanga

 Kijana akiwa na uso wa mshangao baada ya kumuona Dk Magufuli alipokuwa akizungumza na wananchi kabla ya kuvuka Mto Kilombero akitokea wilayani Ulanga kwenda Ifakara

 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli akikagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Kilombero alipokuwa akitoka kufanya kampeni katika Wilaya za Ulanga na Malinyi kwenda   Mjini Ifakara, wilayani Kilombero, Morogoro.







 Mmoja wa wananchi akiwa na bango linalosema Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli anasubiri kuapishwa tu katika mkutano wa kampeni uliofanyika jana Mjini Ifakara, wilayani Kilombero, Morogoro. Dk Magufuli alifanya pia kampeni katika wilaya za Ulanga na Malinyi.  (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)

 Ni furaha iliyoje kwa mwananchi huyu

 Sehemu ya umati wa watu wakati wa kampeni CCM kwenye Uwanja wa Taifa, Ifakara wilayani Kilombero, Morogoro , uliohutubiwa na Mgombea urais wa CCM, Dk John Maguful

 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazee wa CCM, Abdalah Bulembo  akizungumza maneno ya kumnadi Dk Magufuli kabla ya kumkaribisha kujinadi wakati wa mkutano wa kampeni mjini Ifaraka


No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages