Breaking News

Your Ad Spot

Sep 19, 2015

DK. SHEIN AENDELEA NA KAMPENI NA KUSEMA ATAENDELEZA KUUNDA SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA NA KULETA MAENDELEO ZAIDI KWA WAZANZIBAR NA ELIMU BURE

Mgombea Urais wa Zanzibar Kupitia Chama cha Mapinduzi pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Viongozi wa CCM Zanzibar alipowasili katika viwanja vya Mpira Konde Kisiwani Pemba kuendelea na Kampeni Kisiwani Pemba.
Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akiwasalimia Wananchi waliofika katika uwanja wa kunde kuhudhuria mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Shein.wakati akiwasili katika viwanja hivyo vya mpira Konde Wilaya ya Micheweni Pemba.
Wanachama wa CCM Wakimshangilia Mgombea wao wa Urais Dk Shein, wakati akiwasili katika viwanja vya mpira Konde kwa ajili ya mkutano wake wa Tatu wa Kampeni zake kisiwani Pemba.
Taswira ya wakati wa mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais kupitia CCM katika viwanja vya mpira Konde Pemba kama inavyooneka Mwanachama huyu wa CCM akishangilia akiwa na picha ya Mgombea Urais wa CCM Dk Shein.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kaskazini Pemba Ndg Hamad Mberwa Hamad akiwahutubia na kutuoa Sere za CCM zilivotelekezwa na kuiletea Maendeleo Zanzibar katika kipindi chake Dk Shein cha miaka mitano na kuwataka kumpa kura kwa mara ya pili kuendeleza mafanikio ya Maendeleo Zanzibar katika sekta mbalimbali za Jamii Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi Dk Shein akiwana na Viongozi wakifuatilia mkutano huo wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya mpira Konde kisiwani Pemba ikiwa ni mkutano wake wa tatu kisiwani Pemba akiwa katika kampeni zake.
Katibu wa Idara ya Uenezi Afisi Kuu Zanzibar Ndg Waride Bakari Jabu akiwahutubia Wananchi wa Konde katika mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Shein uliofanyika katika uwanja wa mpira Konde Kisiwani Pemba.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages