Baadhi
ya wana CCM na wananchi wakiwa wamefurika katika Viwanja wa Jitegemee
Mjini Muheza ambapo mgombea mwenza nafasi ya urais CCM, Bi. Samia Suluhu
Hassan alifanya mkutano wa kampeni jana.
Baadhi
ya wana CCM na wananchi wakiwa wamefurika katika Viwanja wa Jitegemee
Mjini Muheza ambapo mgombea mwenza nafasi ya urais CCM, Bi. Samia Suluhu
Hassan alifanya mkutano wa kampeni jana.
Mgombea
mwenza wa urais kupitia CCM, Bi. Samia Suluhu Hassan akihutubia umati wa
wanaCCM na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wake wa kampeni
uliofanyika viwanja vya Usagara Tanga Mjini jana. Idadi kubwa ya
wananchi walihudhuria mkutano huo hadi wengine kuzimia kutokana na
msongamano.
Baadhi
ya wana CCM na wananchi wakiwa wamefurika katika Viwanja wa Jitegemee
Mjini Muheza ambapo mgombea mwenza nafasi ya urais CCM, Bi. Samia Suluhu
Hassan alifanya mkutano wa kampeni jana.
Mjumbe
wa Kamati ya Kampeni za CCM Kitaifa, Bi. Ummy Mwalimu akizungumza na
wananchi kwenye moja ya mikutano ya kampeni za CCM timu ya mgombea mweza
iliyofanyika mkoani Tanga jana.(P.T)
Baadhi
ya vijana wakiwa wamepanda juu ya gari ili kumsikiliza mgombea mwenza wa
CCM, Bi. Samia Suluhu Hassan katika Jimbo la Mkinga.
Mgombea
mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimamishwa na wananchi
njiani alipokuwa akielekea katika Jimbo la Mkinga kufanya mkutano wa
kampeni.
Mgombea
mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimamishwa na wananchi
njiani alipokuwa akielekea katika Jimbo la Mkinga kufanya mkutano wa
kampeni.
Sehemu
ya wanaCCM na wananchi ikiwa imemsimamisha barabarani mgombea mwenza wa
CCM, Bi. Samia Suluhu kumsikiliza alipokuwa njiani kuelekea kwenye
mikutano mikubwa ya kampeni. MGOMBEA mwenza wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM), Bi. Samia Suluhu Hassan amevunja ngome ya chama cha ACT Wazalendo
Mkoani Tanga pamoja na kuvuna wanachama 272 kutoka vyama mbalimbali vya
upinzani baada ya wanachama wa vyama hivyo kujiunga rasmi na CCM.
Bi. Samia
Suluhu ambaye ni mgombea mwenza wa Dk. John Pombe Magufuli amefanikiwa
kuvunja ngome za wapinzani jana mjini Tanga katika mikutano yake ya
kampeni baada ya wagombea udiwani watano wa ACT Wazalendo kujiunga na
CCM pamoja na wanachama wengine 235 toka Tanga mjini kujiunga na CCM
kwenye mkutano mkubwa wa kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Usagara
mkoani Tanga.
Akihutubia
katika mkutano mkubwa wa kampeni kunadi ilani ya CCM Tanga mjini uwanja
wa Usagara, Bi. Samia Suluhu aliwapokea wagombea udiwani watano kutoka
ACT Wazalendo, wakiwemo Wilson Elia (wa Kata ya Duga), Gasper Maboko
(Kata ya Nguvumali), Charles Luanda (Maweni) na Marry Scoty (Kata ya
Tanga Sisi) pamoja na Sada Mbwambo (viti maalum).
Mbali na
madiwani hao kukihama chama cha ACT, wanachama 235 kutoka ACT, CUF na
Chadema walijiunga na CCM kwenye mkutano huo wa Tanga mjini huku wengine
37 wakijiunga na CCM katika mkutano mwingine ulofanyika Jimbo la Muheza
hivyo kutimiza wanachama 272 wapya kujiunga katika mikutano ya siku
hiyo.
Akizungumza
na wanaCCM na wananchi waliojitokeza mkutano wa Tanga Mjini, Bi. Suluhu
aliwaomba kuichagua CCM kurudi madarakani ili kuendeleza maendejana
iliyofikia katika maeneo mbalimbali, ikiwemo huduma za kijamii na
miundombinu hasa ya barabara. Alisema wapinzani hawafai kupewa madaraka
kwa kuwa hawajajipanga kimfumo kwani hata viongozi wanaogombea
wamekimbia vyama vyao na wanachotaka ni maslahi yao zaidi.
Alisema
kwa mkoa wa Tanga Serikali ya CCM imepanga kuyakagua mashamba makubwa
yaliotwaliwa na wawekezaji na kutelekezwa kisha kuyarejesha kwa wananchi
ili waweze kuyatumia kwa uzalishaji, ikiwa ni pamoja na kupanua bandari
ya mkoa huo kuchochea maendejana.
Aidha
aliongeza kuwa wakulima wa zao la korosho hawana budi kuongeza
uzalishaji na kutokata tamaa kwani tayari Serikali inafanya mazungumzo
na Serikali ya Norway kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha kubangua
korosho mkoani hapo ili kuongeza thamani ya zao hilo. Alisema lengo la
Serikali ni kuhakikisha asilimia 40 ya vijana wanapata ajira kwenye
viwanda vitakavyo jengwa maeneo anuai ya nchi.
Bi. Samia
alifanya mikutano minne mikubwa katika majimbo ya Mkinga, Pangani,
Mheza na Tanga Mjini na mikutano midogo midongo sita alioifanya njiani
akisimamishwa na wananchi wakitaka kumsikia alipokuwa akipita. Hata
hivyo katika mkutano wake wa Tanga Mjini baadhi ya wananchi walizidiwa
kutokana na msongamano na idadi kubwa ya watu na kuzimia kabla ya kupewa
huduma ya kwanza.
Gari ya
Bi. Samia Suluhu ikitoka kwenye kivuko cha Mv. Pangani II mara baada ya
kuvushwa, mgombea huyo mwenza wa urais CCM alikuwa akitoka kwenye
mkutano wa hadhara JImbo la Pambani jana.
Kutoka kushoto ni mgombea ubunge Jimbo
la Pangani, Jumaa Hamid Aweso, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Pangani,
Hamis Mnegero na Mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Hassan
wakizungumza jambo.
Aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Nkenge, Asumpta Mshama akizungumza na
wanaCCM na wananchi kwenye mikutano ya hadhara jana katika baadhi ya
Majimbo ya Mkoa wa Tanga.
Moja ya ahadi za CCM msimu wa Rais Jakaya Kikwete ikiendelea na ujenzi wa gati Wilayani Pangani ikiendelea na ujenzi
Bi. Samia Suluhu akishuka ndani ya kivuko mara baada ya mkutano wa kampeni uliofanyika Kijiji cha Mwera Jimbo la Pangani.
Bi. Samia Suluhu akihutubia mkutano wa kampeni Muheza.
Baadhi ya wanachama wapya waliojiunga na CCM wakiwa katika msitari mara baada ya kurejesha fomu.
Sehemu ya
wanaCCM na wananchi ikiwa imemsimamisha barabarani mgombea mwenza wa
CCM, Bi. Samia Suluhu kumsikiliza alipokuwa njiani kuelekea kwenye
mikutano mikubwa ya kampeni.
Sehemu
ya wanaCCM na wananchi ikiwa imemsimamisha barabarani mgombea mwenza wa
CCM, Bi. Samia Suluhu kumsikiliza alipokuwa njiani kuelekea kwenye
mikutano mikubwa ya kampeni.
Bi. Samia Suluhu akiwa na mgombea ubunge wa Jimbo la Tanga Mjini Omary Nundu(kulia).
Mmoja wa wananchi wakipewa huduma ya kwanza mara baada ya kuzimia kutokana na msongamano katika mkutano wa kampeni kwa mbaya.
Mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza Tanga Mjini jana.
Mgombea Ubunge wa CCM, Jimbo la Bumbuli, January Makamba akizungumza na wanaCCM na wananchi katika mkutano wa kampeni.
Aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Nkenge, Asumpta Mshama akizungumza na
wanaCCM na wananchi kwenye mikutano ya hadhara jana katika baadhi ya
Majimbo ya Mkoa wa Tanga.
Mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza Tanga Mjini jana.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269