Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari wa NEC, Clarence Nanyaro
Wakati
zaidi ya robo tatu ya vifaa vinavyohitajika vikiwa vimewasili nchini,
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema inaangalia namna ya kuwasaidia
waliopoteza vitambulisho vyao kushiriki kupiga kura.
Kauli
hiyo imetolewa baada ya idadi ya watu wanaotoa taarifa za kupotelewa na
vitambulisho vya kupigia kura pamoja na wanaowasilisha vitambulisho
vilivyookotwa kwa tume kuendelea kuongezeka kila siku licha ya uhakiki
na uhamishaji wa taarifa za mpiga kura kumalizika mapema mwezi huu.
Kaimu
Mkuu wa Kitengo cha Habari wa NEC, Clarence Nanyaro amesema ni
changamoto kwa tume kutokana na wingi wa watu wenye tatizo linalofanana
na hatma yao ya kushiriki uchaguzi mkuu wa Oktoba.
“Kwa wale waliojiandikisha na wakahakiki majina yao lakini wamepoteza vitambulisho tutaangalia namna ya kuishawishi tume itafute jinsi ya wao kushiriki kupiga kura kwasababu majina yao yapo kwenye datfari na yatarudishwa vituoni. Watakachotakiwa ni kuwa na ripoti ya upotevu huo kutoka polisi (Loss report),”
“Kwa wale waliojiandikisha na wakahakiki majina yao lakini wamepoteza vitambulisho tutaangalia namna ya kuishawishi tume itafute jinsi ya wao kushiriki kupiga kura kwasababu majina yao yapo kwenye datfari na yatarudishwa vituoni. Watakachotakiwa ni kuwa na ripoti ya upotevu huo kutoka polisi (Loss report),”
Kitengo
cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) cha tume hiyo
kinaendelea na kupakia taarifa za watu wote waliojiandikisha na Nanyaro
amewatoa shaka wale ambao mpaka sasa wanaambiwa hawaonekani kwenye
kumbukumbu.
Nanyaro amewataka wawe na uhakika wa kushiriki uchaguzi na kubainisha:
“Kuna
wale ambao wakihakiki taarifa zao kwa njia ya simu wanaambiwa
hawatambuliki. Wasiwe na wasiwasi. Kazi ya kuingiza majina yote kwenye
mtandao inaendelea na baada ya muda mambo yatakuwa sawia. Kama
wanavitambulisho, inatosha kuwatambua hivyo wawe na subira’
Imenukuliwa kutoka gazeti la MWANANCHI
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269