Mwenyekiti
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge
(kushoto) akimtambulisha Mgombea Ubunge Jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya
CCM, Mh. Iddi Azzan(kulia) mbele ya umati wa wanachama wa chama hicho
na wananchi waliofurika katika viwanja vya CCM Mwinjuma Mwananyamala
jana jioni.a , wakati wa uzinduzi wa kampeni kwa ajili ya uchaguzi mkuu
wa Oktoba 25, katika jimbo hilo, jijini Dar es Salaam.(Picha na Geofrey
Adroph waPamoja blog)
Mgombea
Ubunge Jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya CCM, Mh. Iddi Azzan akizungumza
na wananchama na wananchi wa maeneo mbalimbali ya jimbo la Kinondoni
waliofurika katika viwanja vya CCM Mwinjuma Mwananyamala jana jioni
wakati wa uzinduzi wa kampeni
Meya wa
Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akihutubia umma uliohudhuria
uzinduzi wa kampeni za mgombea ubunge jimbo la Kinondoni kupitia tiketi
ya CCM.
Meya
mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni, Salum Londa akimwaga sera za CCM mbele
ya umati wa wanachama wa chama hicho na wananchi waliofurika wakati wa
ufunguzi wa kampeni za mgombea ubunge jimbo la Kinondoni zilizofanyika
waliofurika katika viwanja vya CCM Mwinjuma Mwananyamala jana jioni.
Mwenyekiti
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge
akiwasalimia pamoja na kutoa neno kwa wananchama na wananchi waliofika
kwenye mkutano huo wa ufunguzi rasmi wa kampeni za mgembea Ubunge jimbo
la Kinondoni .
Mgombea
udiwani kata ya Mwananyamala Bw. Songoro Mnyonge(kushoto) akitambulishwa
kwa wananchi na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya
Kinondoni, Salum Madenge(kulia)
Mwenyekiti
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge
akimtambulisha Mgombea udiwani wa kata ya Kijitonyama, Ndg. Kamugisha
wakati wa ufunguzi wa kampeni za Mgombea Ubunge jimbo la Kinondoni
Mgombea udiwani kata ya Tandale Bw Tamimu akitema vidonge kwa wapinzani.
Bw. Massawe ambaye ni mgombea udiwani kata ya Ndugumbi akizungumza jambo wakati wa mkutano huo
Mgombea
Udiwani kata ya Magomeni Ndugu Bujugo akiwaomba kura wananchi waliofika
kwenye mkutano huo na pia kuwapigia wabunge pamoja na raisi kupitia
chama cha CCM
Mwenyekiti
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge
(kushoto) akipokea kadi ya CUF toka kwa bibi ambaye alikuwa ni kada wa
chama hicho alidai hajaona manufaa yeyote kuwepo katika chama hicho
ambapo alijitoa rasmi na kurudi CCM.
Bibi akiwasalimia wananchama na wananchi waliofika kwenye mkutano huo
Mzee Dalali akihutubia mamia ya watu waliohudhuria mkutano huo ambao mwenyewe alidai umati ulifikia watu laki 250.
Mgombea Ubunge Jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya CCM, Mh. Iddi Azzan akiendelea kumwaga sera
Umati mkubwa ukishangilia wakati wa mkutano
Baadhi ya wananchi waliofika kwenye mkutano huo
Wasanii wa kizazi kipya Tundaman na Bonge la Nyau wakitumbuiza mara baada ya Mkutani kwisha
Mgombea
Ubunge Jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya CCM, Mh. Iddi Azzan akiaga
mashabiki wake baada ya kumaliza kuhutubia katika viwanja vya CCM
Mwinjuma Mwananyamala jana jioni
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269